Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Jinsi Prof. Bisandu wa Chuo Kikuu anavyowindwa
ElimuHabari Mchanganyiko

Jinsi Prof. Bisandu wa Chuo Kikuu anavyowindwa

Profesa Elifas Bisanda, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)
Spread the love

 

HATUA ya Profesa Elifas Bisanda, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), kutoa waraka wa tahadhari ya maambukizi ya corona, imemuingiza matatani na sasa anawindwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Tayari baraza la chuo hicho limemtaka Prof. Bisanda kuomba radhi kwa kutoa waraka huo kinyume cha taratibu.

Agizo hilo, limetolewa ndani ya saa 48 tangu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kufuta waraka huo uliotolewa na Prof. Bisanda tarehe 8 Februari 2021, kwenda kwa wanafunzi na wafanyakazi wa OUT.

Baada ya kutoa waraka huo, siku moja baadaye (9 Februari 2021), wizara ya elimu ilitoa taarifa kwa umma, iliyosainiwa na Oliva Kato, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa wizara kwamba, tahadhari iliyotolewa Profesa Bisanda ‘ni batili.’

        Soma zaidi:-

“Maelekezo yaliyotolewa na Prof. Bisanda, ambayo ni maoni yake binafsi, hayakuzingatia mwongozo wa udhibiti wa maambukizi ya ugonjwa wa corona katika shule, vyuo na taasisi za elimu nchini wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa tarehe 27 Mei 2020.”

Oliva alisema, wizara inaelekeza wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kuendelea na masomo na kazi zao kama kawaida

Baada ya taarifa hiyo ya wizara, Jumatano tarehe 10 Februari 2021, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Rasilimali, Prof. George Oreku, alitoa taarifa kwa umma kuhusu kikao maalum cha baraza la chuo hicho, kilichokutana jijini Dar es Salaam.

Profesa Oreku alisema, katika kikao hicho cha baraza, kilipokea na kujadili waraka uliotolewa na Profesa Bisanda ambapo “baraza lilibaini sehemu kubwa ya waraka huo ni maoni binafasi ya makamu mkuu wa chuo, pia alikosea kutumia nembo ya serikali.”

Mizengo Pinda, Mkuu wa Chuo Kikuu Huria

“Baraza lilijiridhisha kuwa Profesa Bisanda, alikosea kuandika taarifa husika bila takwimu na kuthibitisha uhalali wa baadhi ya taarifa hizo,” alisema Profesa Oreku.

 

Kutokana na kikao hicho, Profesa Oreku alisema, baraza limetoa maagizo matatu ambayo ni, “makamu mkuu wa chuo (Profesa Bisanda), kuomba radhi kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, mamlaka husika na umma.”

Pia, baraza hilo “linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.”

Maagizo mengine ambayo baraza limetoa ni wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho waendelee na kazi na masomo kama kawaida.

“Manejimenti ya chuo iwakumbushe wafanyakazi na wanafunzi kuhusu miongozo ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) kama ilivyotolewa na serikali,” amesema.

Katika waraka wake Prof. Bisanda, aliandika “naandika hapa kwa uchungu sana, ninapohesabu watu ambao wamefariki katika siku chache zilizopita. Wasomi na wasio wasomi. Wazee na hata vijana. Tutaendelea kupuuzia maelekezo ya viongozi wetu hadi lini?”

Kuhusu kujisomea, makamu mkuu wa chuo hicho alisema “utaratibu ufanyike kuwasaidia wanaotaka kutumia maktaba kama ni lazima, wengi wanaitumia maktaba yetu kama mahali pa kujisomea tu. Maelekezo haya ni kwa ajili ya makao makuu, vituo vyote vya mikoa na vituo vya uratibu vilivyoko nchini.”

Mwisho wa waraka huo, Profesa Bisanda alisema “nimetoa maoni yangu, kama ushauri, nikiwa nawajibika pia kama kiongozi, kuwalinda wale wote ninaowaongoza. Asanteni sana, Mungu awalinde, tumalize huu mwaka salama.”

Profesa Bisanda, aliteuliwa na Mkuu wa chuo hicho, Mizengo Pinda ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu kushika wadhifa huo kwa muhula wa pili na wa mwisho wa miaka mitano kuanzia tarehe 2 Juni 2020.

Muhula wa kwanza wa Profesa Bisanda kama makamu mkuu wa chuo hicho, aliuanza 2 Juni 2015.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!