Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari Majaliwa azungumzia nyongeza ya mishahara
Habari

Majaliwa azungumzia nyongeza ya mishahara

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma, wasikate tamaa kwa vile mishahara mipya haijatangazwa na badala yake amewasihi waendelee kuchapa kazi kwani maslahi yao yanaendelea kuboreshwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

“Nitoe wito kwa watumishi wa umma, wasikate tamaa kwa sababu mishahara mipya haijatangazwa, kikubwa waendelee kuwasilisha hoja zao kupitia mabaraza yao ya wafanyakazi,” amesema.

Majaliwa ametoa wito huo leo Alhamisi, tarehe 11 Februari 2021, wakati akijibu swali la mbunge wa Konde (ACT-Wazalendo), Khatibu Said Haji katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo alitaka kujua ni lini wafanyakazi wa Tanzania watapandishiwa mishahara na kuboreshewa maslahi yao.

“Serikali inayo dhamira na inaendelea na suala la kuboresha maslahi ya watumishi wa umma. Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani ilibaini kwamba ukitangaza kupandisha mishahara, unawaumiza watu wengi wakiwemo wakulima, wafugaji na wavuvi kwani gharama za bidhaa hupandishwa haraka sana,” amesema

Amesema Serikali imejifunza kuwa inapotangaza hadharani kuhusu kupandishwa mishahara, imekuwa inasababisha ugumu wa maisha kwani huduma nyingine kwenye masoko ama usafiri wa mabasi zote zinapanda.

Waziri mkuu amesema, maslahi ya watumishi wa umma hayapo kwenye mshahara peke yake bali pia yanaboreshwa kwa kupunguza kodi na kuwapandisha madaraja.

“Mheshimiwa Rais Magufuli alisema kupandisha mshahara kwa Sh.20,000 au Sh.30,000 haina tija kwa mtumishi bali kupunguza kodi kunamsaidia zaidi mfanyakazi,” amesema.

Esther Matiko

Wakati huohuo, Majaliwa amesema Serikali inapotwaa ardhi ni lazima pafanyike tathmini ili kujua eneo husika lina thamani gani kulingana na mali zilizopo iwe ni nyumba, mazao au kiwanda.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum, asiyekuwa na chama, Esther Matiko kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu bungeni.

Matiko ambaye alifukuzwa Chadema pamoja na wenzake 18, alitaka kujua ni kwa nini tathmini zinazofanyika hazikamiliki na wananchi wakalipwa fidia ili waende sehemu nyingine wakaendelee na shughuli zao.

Waziri mkuu amesema, ardhi ni mali ya Serikali lakini kila mtu anapaswa kuwa na hati ya kutambulisha matumizi ya ardhi anayoimiliki.
“Kila mtu anapaswa kuwa na hati ya kubainisha ardhi anayoimiliki ni ya kitu gani, iwe mashamba, kujenga nyumba au kiwanda,” amesema.

“Kwa hiyo, Mheshimiwa mbunge kama unalo eneo ambalo wananchi wana malalamiko, ni vema uyafikishe kwa viongozi wa eneo husika ili utaratibu wa fidia ufanyike,” amesema Majaliwa

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!