Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Membe: Mkapa alithamini akili kubwa
Habari Mchanganyiko

Membe: Mkapa alithamini akili kubwa

Spread the love

BERNARD Kamilius Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali ya awamu ya nneu, amemtaja Hayati Benjamin William Mkapa, Rais mstaafu wa Tanzania kwamba ni kiongozi aliyethamini akili kubwa. Anaripoti Yusuph Katimba, Dar es Salaam … (endelea).

Mkapa alifikwa na mauti Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam kwa mshtuko wa moyo. Aliongoza Tanzania kwa miaka kumi mfululizo kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

Akizungumza katika uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, mahala ambapo misa ya kumwombe Mkapa (81) imefanyika leo Jumapili tarehe 26 Julai 2020, Membe amesema Mkapa alimpa heshima kila kiongozi aliyekuwa akitumikia wananchi.

“Rais Mkapa, siku zote alikuwa anathamini akili kubwa, yaani kutumia maarifa katika kuongoza. Alikuwa anathamini nidhamu ya kazi na alikuwa anathamini utekelezaji wa sera, sio mtu,” amesema Membe.

        Soma zaidi:-

Akizungumzia barua aliyoandikiwa na Mzee Mkapa Januari 2020, Membe amesema, alielezwa kwamba binadamu ameumbwa kwa ajili ya kutumikia wengine. Na kwamba, anathamini sana binadamu anayefanya kazi kwa ajili ya watu wengine.

“Kwenye barua ile alieleza, binadamu umeumbwa kwa ajili ya kutumikia wananchi na yeye anathamini sana mtu anapokuwa duniani anapotumikia watu wake,” amesema.

Amemweleza Mkapa kwamba alilelewa kwenye familia ya maadili na kuwa, hata alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado aliishi maisha aliyolelewa na baba yake.

Membe amesema, “Mzee Mkapa atakumbukwa kwa uchapaji kazi wake, alikuwa mpatanishi na aliheshimika sana na viongozi wastaafu wa Bara la Afrika.”

“Mara nyingi alikuwa akizungumzia matatizo ya Bara la Afrika na kufikia muafaka katika suala la migogoro,” amesema Membe ambaye ni mtia nia wa urais wa Tanzania kupitia chama cha siasa cha upinzani ACT-Wazalendo.

“Tumempoteza kiongozi ambaye ametumia maisha yake yote katika kusaidia wanachi. Mzee Mkapa alikuwa anathamini sana dini na akawa muumini mkubwa sana wa dini ya Kikristo.”

Mkapa aliyezaliwa tarehe 12 Novemba 1938 atazikwa Jumatano tarehe 29 Julai 2020 kijijini kwake, Lupaso Mkoa wa Mtwara.

1 Comment

  • pmzka mzee,vip sera yako ya uwazi Na ukweli itaenziwa, chama umekiacha vibaya,mtu aneza iba hela huko anakuja waonga wajumbe anaptshwa Na kuingia bungeni Na kfcha zambi zake humo Na aliowatapeli wananymaza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!