Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Ndugulile: Msiache mbachao kwa msala upitao
Habari za Siasa

Dk. Ndugulile: Msiache mbachao kwa msala upitao

Dk. Faustine Ndugulile
Spread the love

DAKTARI Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni anayemaliza muda wake amesema, bado ana mikakati ya kuendelea kutatua changamoto ndani ya jimbo hilo. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Ndugulile amesema hayo leo Jumatatu tarehe 20 Julai 2020 katika mkutano mkuu wa jimbo la Kigamboni wenye lengo la kupiga kura za maoni kumpata mgombea ubunge.

Katika kitabu cha wagombea, Dk. Ndugulile anayetetea nafasi hiyo ni mgombea namba 58 kati ya 78 wanaowania kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

        Soma zaidi: 

Akijinadi mbeye ya wajumbe wa mkutano huo unaofanyikia ukumbi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kuvukoni amesema, “mlinipa imani ya kuwa mbunge na nikawapa utumishi na sasa nawahakikishia tena mnipe imani ili niwape tena utumishi. Msiache mbachao kwa msala upitao,” amesema.

Ameeleza mbele ya wajumbe hao kuwa katika kipindi cha uongozi wake, amefanikiwa kujenga mfumo nzuri wa afya pamona na elimu katika jimbo na kuwa katika matokeo ya shule ya msingi ya mwaka huu Kigamboni imeshika nafafi ya 10 kitaifa.

Paul Makonda

“Nakiri kwamba, pamoja na yote yaliyofanyika bado kuna changamoto mbalimbali na bado nina mikakati ya kuzitatua,” amesema. 

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV  kwa habari zaidi

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!