ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Paul Makonda amesema ana uwezo wa kuyatekeleza yale yote yaliyomo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na yakatokea. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).
Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 20 Julai 2020 katika mkutano mkuu wa CCM Jimbo la Kigamboni, Dar es Salaam unaofanyikia ukumbi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kuvukoni wenye lengo la kupiga kura za maoni jimbo hilo.
Wagombea watakaopigiwa kura ni 78 akiwemo mbunge anayemaliza muda wake, Dk. Faustine Ndugulile.
Akijinadi kwa wajumbe wa mkutano huo, Makonda amesema, “najua changamoto tulizonazo, ninao uzoefu wakutosha na si tu kwa kuongoza bali kwa kutatua changamoto, ninayo picha ya changamoto zote za Jimbo kwakuwa nilikuwa kiongozi ndani ya chama.”

“Nimepita na nimeona hali ambayo hairidhishi ya ofisi zetu, nitahakikisha kila kata iwe na mfuko wake au Saccos yake ili kumwezesha kiongozi husika afanye kazi kiwepesi.”
Makonda ni mgombea namba 38 katika kitabu cha wagombea ambapo kwa mujibu wake mwenyewe amewaambia wajumbe kuwa wakisahau jina lake kwenye kumpigia kura basi wakumbuke miaka ambayo ameitaja kuwa ni 38.
Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi
Leave a comment