Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Corona yaendelea kuitesa Kenya, vifo vyafikia 137
Kimataifa

Corona yaendelea kuitesa Kenya, vifo vyafikia 137

Spread the love

SERIKALI ya Kenya imeripoti wagonjwa wapya 149 wa virusi vya corona (COVID-19) baada ya kupima sampuli 3,090 ndani ya saa 24 zilizopita. Anaripoti Mitandao ya Kimataifa  … (endelea)

Maambukizo yamefikia 5,533 na vifo vimeongezeka na kufikia 137 baada ya wagonjwa watano kufariki dunia.

Wagonjwa 48 wameruhusiwa kutoka Hospitalini na kufanya idadi ya waliopona ugonjwa huo kufika 1,905.

Kenya imekuwa na utaratibu wa kutoa taarifa kila siku za corona ambapo leo Ijumaa tarehe 26 Juni 2020, naibu waziri wa afya wan chi hiyo, Dk. Rashid Aman kati ya wagonjwahao 149 wapya, 148 ni Wakenya na mmoja ni raia wa kigeni.

Amesema, wanaume ni 94 na wanawake ni 55 wenye umri kati ya miaka 76.

Dk. Aman amesema, kati ya wagonjwa hao 149; Nairobi (73), Mombasa (20), Kajiado (15), Siaya (13), Machakos (3), Kilifi (1), Nakuru (1), Nandi (1), Bungoma (1), Isiolo (1).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!