Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Jiji la Dodoma kugawa maeneo kwa mtandao, kisa Corona
Habari Mchanganyiko

Jiji la Dodoma kugawa maeneo kwa mtandao, kisa Corona

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi
Spread the love

KUTOKANA na tishio la ugongwa hatari wa Coroma, halmashauri ya jiji la Dodoma limetoa utaratibu wa kuomba maeneo ya biashara kwa njia ya mtandao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesena kutokana na kuwepo kwa msongamano wa waombaji wa maeneo ya biashara ofisini kwake, sasa fojunza maombi zitatolewa kwa njia ya mtandao.

Kunambi alisema maeneo yanayoombwa kuwekezwa na wafanyabiashara ni Soko la Ndugai, Standi mpya ya Mabasi na eneo la mapumziko Chinangali Park.

Alisema wakati wanaandaa utaratibu wa uchukuaji wa fomu hizo kwa njia foleni hawakutarajia kama muitikio utakuwa mkubwa lakini wananchi walijitokeza kwa wingi hali iliyosababisha wao kuamua kusitisha utaratibu huo.

Pia Kunambi alisema kuwa jiji linaendelea na uuzaji wa viwanja katika maeneo mbalimbali ikiwemo viwanja vya ujenzi wa hoteli, majengo makubwa na viwanda.

Alisema wameandaa utaratibu mpya ambao utaondoa msongamano lakini pia utamuwezesha kila mwananchi aliye popote nchini kupata fomu bila kusafiri na bila urasimu wowote.

Kunambi alisema utaratibu huo unatarajiwa kuanza rasmi April 13 mwaka huu, ambapo utakuwa ni uchukuaji wa fomu kwa njia ya mtandao, huku akiwataka wananchi kufuatilia kwenye website ya jiji la Dodoma kwa kuanzia siku hiyo.

Aidha alisema wananchi ambao tayari wameshachukua fomu April 7 mwaka huu kwa kutumia utaratibu wa awali, wataingizwa kwenye mfumo moja kwa moja na watatambulika kwa sababu tayari ni wateja wao.

Hata hivyo alisema anawasihi watanzania waondokane na dhana kuwa kuna watu maalum au wenye fedha ndio watakaofanikiwa kupata nafasi hizo za kufanyia biashara.

Alitaja maeneo ambayo viwanja hivyo vinauzwa ni Njedengwa Investment Center na tayari kuna huduma zote za kijamii na viwanja vya Ujenzi wa Viwanda katika eneo la Nala kilomita 20 kutoka mjini.

Kunambi, alivitaja viwanja vingine kuwa ni viwanja vya makazi vilivyopo katika eneo la Mtumba, Choigongwe, Kikombo na Mapinduzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!