Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Watanzania wabuni kifaa cha kutambua homa kali
Habari Mchanganyiko

Watanzania wabuni kifaa cha kutambua homa kali

Spread the love

KAMPUNI ya Emotec, inayomilikiwa na Mtanzania imebuni mfumo wenye uwezo wa kutambua mtu mwenye homa kali ikiwemo muathirika wa virusi vya corona (COVID-19), ndani ya muda mfupi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa teknolojia hiyo, leo tarehe 7 Aprili 2020 jijini Dar es Salaam, Moses Hella, mkurugenzi wa kampuni hiyo, amesema mfumo huo unafanya kazi pindi unapowekwa katika kamera.

Hella amesema, kamera yenye mfumo huo, ina uwezo wa kutambua watu wengi wenye homa kali, ndani ya muda mfupi. Na kuwa hutambua joto la mtu mmoja ndani ya sekunde chache.

“Sasa hivi mtu anawekea kipimo karibu sana kitendo ambacho ni hatari. Kutokana na hilo tumewaletea kamera hizi ambazo zinaweza kutambua joto la mtu, kutoka umbali wa kutosha. Kamera ionyesha mfano yule mwenye nguo fulani ana joto lisilo la kawaida.

Inaweza kumtambua kila mmoja kwa sekunde, na kutambua watu wengi kwa wakati mmoja,” amesema Hella.

Hella amesema EMOTEC imeamua kuvumbua teknolojia hiyo, ili kuunga juhudi dhidi ya mapambano ya kudhibiti ueneaji wa virusi hivyo.

“Hizi camera zinaweza kuwa mbalu mita 1.5, wakati vile vifaa vya kupima, mtumishi huw karibu zaidi, lazima umsogelee zaidi mhusika. Ni hatari zaidi,” amesema Hella.

Hella amesema kamera hizo zinauzwa kulingana na ubira wake, ambapo kima cha chini, inauzwa kuanzia Sh. 1 milioni.

“Zipo kamera za kushika mkononi zenye uwezo wa kutambua umbali mrefu na za kufunga. mara nyingi kamera hizi zinatumika maeneo yenye mkusanyiko,” amesema Hella.

Wakati huo huo, Hella amesema kampuni yake imebuni kamera kwa ajili ya ulinzi wa nyumba na kwenye sehemu za biashara.

Amesema, kamera hizo zina uwezo wa kutoa taarifa pindi linapotokea tatizo katika nyumba ilizofungwa.

Amesema, mmiliki wa kamera hizo ana uwezo wa kuzungumza na mgeni aliyeko nje, huku yeye akiwa ndani.

“Kwa wafanyabaishara, umeajiri watu tunakupa kifaa cha kufungua milango. Ambacho hakitumii nyilwa ‘password’. Kwa kuzingatia changamto hii, tumebuni kifaa kinachofungua kulingana na sura ya mtu ambaye imeorodheshwa katika kifaa hicho.

“Pia, tunawafungia kamera ambazo zina uwezo mkubwa zaidi ya nyumbani. Zina uwezo wa kutambua kitu fulani kimeingia na kutoka, zina uwezo wa kutambua kama ni gari au mtu na kama ni kiumbe kisicho na athari, haiwezi piga kelele,” amesema Hella.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!