Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Sheikh akerwa na vinara wa migogoro Bakwata
Habari Mchanganyiko

Sheikh akerwa na vinara wa migogoro Bakwata

Spread the love

SHEIKH wa Mkoa Dodoma, Alhajji Sheikh Mustafa Rajabu Shabani, amesema amechukizwa na baadhi ya viongozi ndani ya Baraza la Waisilamu (BAKWATA) Mkoa na Wilaya kuwa vinara katika kuchochea migogoro. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma …  (endelea).

Mbali na kuchukizwa na vitendo hivyo kiongozi huyo, amesema kuwa watu ambao wanasababisha kuwepo kwa migogoro ndani ya misikiti na kutoiheshimu katiba ya Bakwata watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Sheikh Alhaji Rajabu ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na viongozi katika kikao cha Mkutano mkuu wa uchaguzi wa Baraza la Waisilamu BAKWATA Wilaya ya Dodoma ngazi ya Wilaya.

Katika mkutano huo ulioambatana na uchaguzi wa Mwenyekiti Bakwata, Wajumbe wa Halmashauri ya Bakwata Wilaya na Baraza la Mashek Bakwata Wilaya Sheikh wa Mkoa alisema kuwa imezuka kasumba ya baadhi ya viongozi ndani ya Bakwata kuwa chanzo cha migogoro ndani ya dini hiyo.

Kutokana na hali hiyo kiongozi huyo amewaonya wajumbe wa halmashauri ya Wilaya ya Dodoma mjini kutowachagua viongozi ambao watakuwa vimeo katika uongozi na kusababisha kuwepo kwa migogoro ambayo kimsingi hurudisha nyuma maendeleo.

“Kumekuwepo na tabia ya kuwachagua viongozi vimeo ambao badala kujenga umoja, mshikamano na upendo kwa nia ya kujenga maendeleo wao wamekuwa kinyume, kwani wamekuwa chanzo cha fujo ndani ya misikiti.

“Siyo siri na ninawatambua viongozi ambao walikuwa katika baraza la halmashauri ya Bakwata Mkoa lakini cha kushangaza wamekuwa chanzo kikubwa cha kuzua migogoro kwa maana hiyo nawaomba wapiga kura kuwabwaga watu hao na kuwachagua watu makini wenye nia ya kulifanya baraza la Bakwata Wilaya kusomba mbele,” alisema Sheikh wa Mkoa.

Kwa Upande wake mgeni rasmi katika Mkutano huo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde aliwataka viongozi na waumini wa dini ya Kiislamu kuhakikisha wanaheshimu katiba yao pamoja na kuwa waadilifu kwa viongozi wanaowaongoza.

Mavunde alisema kuwa vitabu vitakatifu vinatambua kuwepo kwa viongozi, kufuata sheria ya dini na serikali pamoja na kuwa watii kwa kilajambo jema ambalo linatakiwa kifanyika kwa maendeleo ya dini ya uislamu na maendeleoya kijamii.

Mbunge huyo alisema Baraza la Bakwata linatakiwa kuwa na viongozi makini na wasiokuwa na chambe yoyote ya kusababisha vurugu na kuuchafua Uislamu badala yake wanatakiwa kujenga Umoja, Upendo na Mshikamano katika kukuza Uislamu na na Kuchochea Maendeleo.

Baada ya uchaguzi Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Halmashauri ya Bakwata Wilaya ya Dodoma Ustadhi, Bashiru Hussein, alisema kuwa katika nafasi yake aliyopatiwa na wajumbe itakuwa ni nafasi ya kuwaunganisha waislamu wote wa Wilaya na kuwafanya kutambua kuwa Bakwata ndicho chombo pekee cha kuwaunganisha waislamu wote nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!