CHAMA cha NCCR- Mageuzi, kimekana madai kuwa kimetumia kiasi Sh. 1.19 bilioni, zilizotolewa na serikali, bila kuwa na uthibitisho wa nyaraka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katibu mkuu wa chama hicho, Elizabeth Mhagama amesema, chama chake kinapokea ruzuku ya chini ya Sh. 3.5 milioni kwa mwezi, na hivyo, kwa vyovyote vile, “hakiwezi kutumia mabilioni hayo ya shilingi.”
Mhagama ametoa kauli hiyo, katika mahojiano yake na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu jana Jumatano. Alikuwa akijibu madai yaliyokuwa yametolewa na wakili mashuhuri wa mahakama kuu, Fatma Karume.
Akiandika katika ukurasa wake wa twitter, Fatma ambaye anafahamika pia kwa jina la Shangazi amekituhumu chama hicho, kwa kile alichodai, “matumizi mabaya ya fedha za umma.”
Amesema, “sikuweza kustahimili mpaka kesho. NCCR- Mageuzi na CUF (Chama cha Wananchi), wamepewa adverse (reports – report mbaya) na CAG (Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali).”
Anaongeza: Sababu, NCCR wametumia zaidi ya Sh. 1.19 bilioni, bila kuwa na uthibitisho. Nayo CUF pia hawana vithibitisho ya matumizi ya zaidi ya Sh. 580. Wache waunge mikono juhudi tu.”
Kwa mujibu wa ripoti ya CAG inayoeleza hali ya vyama vya siasa, chama cha NCCR- Mageuzi, tofauti na anavyoeleza Fatma Karume, chama hicho, kimetumia kiasia cha Sh. 1,190,250 tu.
Leave a comment