Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata Meya Dar: CCM waufyata
Habari za SiasaTangulizi

Sakata Meya Dar: CCM waufyata

Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam akiwa ofisini kwake kuendelea na kazi
Spread the love

WAJUMBE wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wameshindwa kuendelea na mkakati wao wa kumng’oa Isaya Mwita, Meya wa jiji hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu, leo tarehe 15 Januari 2020, Meya Mwita amesema anaendelea majukumu yake ya kazi kama kawaida, baada ya kurejeshewa nywila (password) ya kuingilia ofisini kwake, iliyobadilishwa na baadhi ya wajumbe wa halmashauri ya jiji hilo, kutoka CCM.

Tarehe 13 Januari mwaka huu, Meya Mwita alishindwa kutekeleza majukumu yake, baada ya password ya kuingia ofisini kwake kubadilishwa, siku kadhaa baada ya Wajumbe wa Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo kutoka CCM, kutangaza kumvua madaraka.

“Mimi nachokumbuka nilivyokwenda baada ya mlango kufungwa, walikuja kufungua na nikaendelea majukumu yangu ofisini. Na bado naendelea na majukumu yangu,” ameeleza Meya Mwita.

Aidha, Meya Mwita amemuomba Sipora Liana, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kumrejeshea gari yake ya ofisi.

“Mkurugenzi wa jiji alichukua gari yangu, sijaona gari hadi sasa, waambieni wanirudishie ninakazi nayo,” amesema Meya Mwita.

Akizungumzia sakata hilo, Meya Mwita amesema amewasamehe wote waliohusika kusuka figisu hizo, na kwamba hana kinyongo nao.

“CCM ndiyo wanasema nimenyang’anywa umeya, unadhani wataongea nini? Hakuna mtu wa kuniondoa, kama kuniondoa wataniondoa kwa kanuni zilizowekwa. Na kanuni zinasema wanatakiwa wapate wajumbe 2/ 3 hawakupata sasa nani anaweza kuniondoa umeya?” amehoji Meya Mwita na kuongeza;

“Nimewasamehe nipo tayari kupiga kazi kama zamani sina kinyongo nao. Waje tuendelee kuwatumikia wananchi wa Dar es Salaam.”

Tarehe 9 Januari 2020, kilifanyika kikao kilichokuwa na agenda ya kujadili tuhuma zilizokuwa zinamkabili Meya Mwita, ikiwemo za matumizi mabaya ya ofisi, kwa ajili ya kumchukulia hatua.

Lakini kikao hicho kiliibua vurugu, baada ya wajumbe wa upande wa upinzani kupinga mchakato uliotumika kuendesha kikao hicho, kilichotangaza kumvua madaraka Meya Mwita.

Wajumbe hao walipinga kikao hicho kwa maelezo kwamba, hakikutimiza akidi ya wajumbe, pamoja na kughushi saini ya mjumbe mmoja, ambaye hakuwepo katika kikao hicho.

Baada ya mkanganyiko huo, kesho yake, tarehe 10 Januari mwaka huu, Meya Mwita alienda ofisini kwake kwa ajili ya kuendelea na majukumu yake ya kazi, akisema kwamba bado ni meya halali wa jiji hilo, kwa kuwa mchakato uliotumika kumng’oa haukuwa halali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!