October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtumishi TPA kizimbani kwa Utakatishaji wa Bil. 5.8

Spread the love

ALIYEKUWA Mfanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Stephen Mtui amefikishwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi mbili Ikiwemo utakatishaji fedha kiasi cha shilingi bilioni 5.8. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka hayo leo na Wakili wa Serikali, Faraji Nguka mbele ya Hakimu, Vicky Mwaikambo na kuunganishwa na wenzake wawili ambao tayari wameshasomewa mashtaka yao Desemba 13 mwaka 2019 mahakamani hapo. 

Katika shtaka la wizi akiwa mtumishi, inadaiwa kati ya Julaj 2014 na April 2015 akiwa na wenzake Merina Chawala na Happygod Ulomi katika bandari kavu ya AMI Jijini Dar es Salaam waliiba kiasi cha Sh. 5.4 bilioni ambayo ni mali ya TPA.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Mtui anakabiliwa na kosa la kuisababishia Mamlaka hasara ambapo kati ya Julai 2014 na Aprili 2015 ndani ya jiji la Dar es Salaam aliisababishia TPA hasara ya zaidi ya Sh. 5 bilioni.

Pia, shtaka la kugushi, mshtakiwa kati 2014 na 2015 katika tarehe tofauti anadaiwa kutengeneza hati ya malipo ya Sh. 10 milioni kuonyesha kuwa bandari kavu ya DCID na AMI kupitia benki ya CRDB zimeilipa TPA kiasi hicho huku ikiwa si kweli.

Katika shtaka la wizi akiwa mtumishi, katika nyakati tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam mshtakiwa akiwa mfanyakazi wa CRDB akishirikiana na wenzake, wanadaiwa kuiba jumla ya dola za kimarekani 17,993.26 ambazo ni mali ya TPA.

Katika kosa la utakatishaji fedha, kati ya Julai 2014 na April 2015 mshtakiwa pamoja na wenzake sita wanadaiwa kujipatia zaidi ya Sh. 5 bilioni, huku wakijua fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi.

Kesi nyingine Mtui anadaiwa kuisabababishia Mamlaka ya bandari hasara ya Sh. 448 milioni, ambapo akiwa mtumishi wa mamlaka hiyo.

Mbali na kutakatisha fedha Wakili wa Serikali Nguka Mbele ya Hakimu Mwaikambo amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na mshtaka 19 ya wizi, mashtaka matano ya kughushi na moja wezi akiwa mtumishi.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Wakili Nguka ameeleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi ambayo pia haina dhamana.

Katika shauri hilo, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Valentino Sangawa Mhasibu TPA, Leticia Massaro mfanyakazi wa TPA Christina Temu karani wa TPA na wafanyakazi wa CRDB Eva lihokolelo, Lenfrida Magawa

Kesi imeahirishwa hadi tarehe 30 Januari, 2020 ambapo mshtakiwa amerudishwa mahabusu.

error: Content is protected !!