Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kampuni yaingia mitini na Mil 200 za wakulima wa zabibu
Habari Mchanganyiko

Kampuni yaingia mitini na Mil 200 za wakulima wa zabibu

Spread the love

ZAIDI ya wakulima 26 wa zabibu wameilalamikia kampuni ya Dane Holdings Limited ya Nkulabi Village kwa kutowalipa fedha zao zaidi ya Sh. 200 milioni wanazodai. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wakulima hao wakizungumza na vyombo vya habari jijini hapa wamesema kuwa ni zaidi ya miezi minne sasa toka waiuzie kampuni hiyo zabibu lakini hawajalipwa fedha zao.

Walisema kuwa waliiuzia kampuni hiyo zabibu toka mwezi wa nane mwaka huu lakini wamekuwa wakizungushwa bila mafanikio jambo ambalo linawafanya kuwa na Maisha magumu.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima, Veronika Mkunda alisema kutokana na wakulima hao kutolipwa fedha zao kwa wakati kumesababisha wakulima kuwa na Maisha mabaya.

“Sisi ni wakulima na tumeiuzia kampuni zabibu ili kujikimu na matatizo mbalimbali lakini cha kushangaza hatujalipwa kwa wakati.

“Kutokana na hali hiyo maisha yetu yamekuwa mabaya, tunashindwa hata kuandaa mashamba, tunajiandaa kulipa ada za watoto shule hatujui tutafanyaje, lakini pia huu ni msimu wa sikukuu tutawezaje kujikimu.

“Kwa mazingira haya sasa tunaiomba serikali kuingilia kati suala hili ili tuweze kulipwa fedha zetu na tuendelee na shughuli nyingine za kuandaa mashamba,” alisema Veronika.

Mbali na kutolipwa fedha zao wakulima hao pia wameiomba serikali kuwatafutia masoko ya uhakika ili waondokane na tatizo la kuuza zabibu kwa mkopo.

Wamesema kuwa wanajikuta wakiyakopesha makampuni na wakati huo wanatumia gharama kubwa kuandaa mashamba jambo ambalo linakatisha tamaa.

Pia wakulima hao walisema licha ya kuwa kilimo cha zabibu kuwa cha gharama lakini wakulima hawanufaiki kutokana na wakulima kukosa soko la uhakika.

Veronika alisema kuwa kutokana na kukosekana kwa soko la zabibu wanunuzi wamekuwa wakijipangia bei wanayoitaka jambo ambalo linamfanya mkulima kuendelea kuwa masikini.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Dane Holdings Limited ya Mkulabi Village, Mhandisi Danford Semwenda alisema kuwa ni kweli wakulima hao wanadai zaidi ya Sh. 200 milioni.

Hata hivyo Semwenda alisema kuwa ifikapo Januari 8 mwaka kesho wakulima hao watakuwa wamelipwa fedha zao zote kwani hata yeye kuna fedha anadai lakini hajalipwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!