Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwambe ameonja sumu kwa ulimi
Habari za Siasa

Mwambe ameonja sumu kwa ulimi

Cecil Mwambe,, Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jimbo la Ndanda, mkoani Mtwara,
Spread the love

IMBUNGE wa Chadema, katika jimbo la Ndanda, wilayani Masasi, mkoani Mtwara, Cecil David Mwambe (45), amethubutu. Amejaribu na ameweza kutenda kile kilicho washinda wengi. Anaandika Joseph Mwanakijiji, kada wa Chadema.

Amejitosa katika vita ya kuwania “uenyekiti wa Freeman Mbowe,” ndani ya chama chake. Hakika, hili halikuwa jambo dogo. Ni hatua kubwa mno na inayopaswa kupongezwa. Waliokuwa wanamuunga mkono wanasema, “Mwambe ameonya sumu kwa ulimi.”

Kabla ya kufikia hatua hiyo, mwanasiasa huyo, amepitia mabonde na milima. Amepachikwa majina lukuki, yakiwamo; “msaliti, shipa na wakala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anayetumika kumuondoa Mbowe.”

Lakini mwenyewe amejitahidi sana kujizuia kujibu tuhuma hizo. Amekuwa akiishia kusema, “kumpinga Mbowe, siyo usaliti.” Ni haki yake ya kikatiba.

Pamoja na kushindwa uchaguzi mkuu wa jana, Mwambe ameacha funzo kubwa ndani ya chama la uvumilivu, busara na hekima. Vinginevyo, ngumi zingepingwa na baadhi ya vikao vya Kamati Kuu (CC), ambayo yeye alikuwa mjumbe, vingevunjika.

Hata hivyo, lililokubwa zaidi, ni kwamba Mwambe amemuachia mwenyekiti wake, msala mzito na kwa mara ya kwanza, Mbowe anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuendelea kukubalika ndani ya chama chetu hasa kwenye maamzi ya jumla kwenye chaguzi za ndani.

Hii ni kwa sababu, katika kampeni zake, Mwambe ametumia kauli ambazo zitaendelea kukumbukwa na wapigakura wengi na zitaweza kuchochea mabadiliko ndani ya chama.

Kwa mfano, Mwambe ameeleza hoja ya kulipa watendaji wake kwenye ngazi za wilaya, mikoa na mabaraza, angalau posho ya kila mwezi.

Hili halijawahi siyo kutendwa na uongozi wa Mbowe, bali hata kusemwa. Pamoja na Chadema kukusanya mamilioni ya fedha yanayotokana na ruzuku na michango ya wanachama, hakuna mtendaji hata mmoja, ukiondoa wale wa makao makuu na kanda, wanaolipwa ujira.

Taarifa zinasema, Chadema kimeweza kukusanya takribani Sh. 15 bilioni, katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa Mbowe.

Aidha, Mwambe amesema, alikuwa analenga kung’atua madaraka kwenye Kanda, mikoa na wilaya. Kwa sasa, kila kitu kinafanywa na makao makuu.

Amezungumzia pia mabadiliko ya sekretarieti ya chama chake. Akawatuhumu waliopo kuwa ndio chanzo cha kuzorota kwa chama. Akasema, sektarieti iliyopita, haijaweza hata kukusanya matokeo ya uchaguzi mkuu uliyopita.

Amezungumzia kuboresha posho za wajumbe vikao vya chama, ikiwamo Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkutano. Kwa sasa, wajumbe hao wanalipwa kati ya Sh. 30,000 na 100,000 (laki moja). Yeye alipanga kuwalipa kati ya Sh. 50,000 na 150,000 (laki moja na nusu).

Lakini kubwa zaidi, Mwambe amezungumzia uwazi kwenye ruzuku ya chama. Uongozi wa Mbowe, unatuhumiwa pamoja na mengine, kutokuwapo kwa uwazi huo.

Ndio maana baadhi ya wachambuzi wa masuala ya fedha wanahusisha kukoseka huko kwa uwazi, kuwa chanzo cha chama hicho, kupata hati chafu mwaka jana.

Ameweza kushawishi kwa kiwango kikubwa hoja ya Chadema ya kuwa na jengo lake la makao makuu lenye hadhi na bora. kwa matumizi ya makao makuu. Majengo ya sasa yanayotumiwa na chama hiki – moja limenunuliwa na uongozi wa uenyekiti wa Bob Makani na katibu mkuu, Dk. Warid Kabour na jingine limekodishwa.

Kwa mujibu wa Mwambe, hayo na mengine yakiweza kutekelezwa yatakisaidia chama kuwa na mashineli yake. Itakijenga na kuwa taasisi; tofauti na sasa ambako mwenyekiti wa chama ndio kila kitu.

Ni kazi ya Mbowe sasa kutekeleza kile ambacho Mwambe amekisema na ambacho kimekuwa kikisemwa kwa siku nyingi, ingawa chini kwa chini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!