Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mnyika Katibu Mkuu Chadema, Mbowe ampoza Heche
Habari za SiasaTangulizi

Mnyika Katibu Mkuu Chadema, Mbowe ampoza Heche

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amemteua John Mnyika, Mbunge wa Kibamba kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho na kuchukua nafasi ya Dk. Vincent Mashinji aliyemaliza muda wake. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe pia amemteua kwa mara nyingine Salum Mwalimu, kuendelea kuwa Naibu Katibu Mkuu Z’bar, wakati Benson Kigaila anakuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, akichukua nafasi ya Mnyika aliyeteuliwa Katibu Mkuu. 

Katika teuzi hizo, Mbowe amepoza machungu ya John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini ya kushindwa katika uchaguzi wa Kanda ya Serengeti kwa kuangushwa na Ester Matiko, kwa kumteua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.

Mbowe amesema amewateua makatibu hao pamoja na Heche kwa kuwa ana mapenzi na chama chake, kwani anaamini viongozi wao watamsaidia katika kukipeleka mbele chama hicho hasa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

“Sina maana niliowachagua ni bora kuliko waliomaliza muda wao, lakini lazima wachache wawe mbele kuwaongoza wengine,” alisema Mwenyekiti Mbowe.

Katika mkutano huo pia kulikuwa na uchaguzi wa wajumbe nane wa Kamati Kuu kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na kundi linalowakilisha walemavu.

Akitangaza matokeao hayo, Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake, Vincent Mashinji, amesema katika kundi la Wajumbe wa Kamati Kuu wanaowakilisha Zanzibar, kura zilizopigwa ni 405, kura halali ni 403, mbili zimeharibika, mshindi ni Yahaya Alawi Omari amepata kura 278 sawa na 68.64% wakati Hemed Ali Hemed aliyepata 125 sawa 30.86%.

Katika Wajumbe wanawake kutoka Zanzibar kura zilizopigwa ni 390, 15 zilizoharibika, mshindi ni Zeud Mvano Abdurah aliyepata kura 319 sawa na 78.8% dhidi ya Zainab Mussa Bakari aliyepata kura 39 sawa 9.6% na Sharifa Suleiman aliyepata kura 32 sawa 7.9%.

Wajumbe wanaowakilisha kundi la walemavu mshindi ni Sara Abdallah Katanga aliyepata kura 265 sawa na 65.5% dhidi ya Samson Nelson Mwambwene aliyepata kura 140 sawa 34.5%.

Wajumbe wa Kamati Kuu wanaume Tanzania Bara, washindi ni Patrick Ole Sosopi aliyepata kura 325 sawa na 74%, Ahobokile Michael Mwaitenda aliyepata kura 272 sawa na 67% na Gipson Braisius Meseyeki aliyepata kura 264 sawa na 65% dhidi ya Meshard Lwizire Tiba aliyepata kura 221 sawa na 54%.

Kwa upande wa Wanawake Tanzania Bara washindi ni Suzan Limbeni Kiwanga aliyepata kura 300 sawa na 74.6% na Grace Sindato Kihwelu aliyepata kura 262 sawa na 65%, dhidi ya Pamela Simon Maasy aliyepata kura 257 sawa na 63.9%, Ester Cyprian Daffi aliyepata kura 158 sawa na 39.3%, Catherine Varence Vermand aliyepata kura 129 sawa na 32% na Beth Donatus Masanja aliyepata kura 29 sawa na 7.2%.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

error: Content is protected !!