Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Michezo Gidabuday aweka wazi sababu ya ya kujiuzuru RT
Michezo

Gidabuday aweka wazi sababu ya ya kujiuzuru RT

Spread the love

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Riadha Tanznia (RT), Wilhelim Gidabuday amejiuzuru nafasi yake kwenye shirikisho hilo baada ya kushaulina na kukubaliana na kamati tendaji kwa maslahi mapana ya shirikisho hilo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kidabuday amechukua uamuzi huo jana baada ya kufanya kikao cha muda mrefu na maamuzi yake kukubaliwa na kamati tendaji ya shirikisho huku akiahidi kuendeleza ushirikiano na viongozi waliobaki.

“Sababu ya mimi kujiuzuru mbele ya kamati ya utendaji kwa ajili ya maslahi mapana ya shirikisho la riadha, siyo kwamba niliowaacha ni wabaya ila ile njia nilioitaka mimi haijaungwa mkono na wengi,” alisema Kidabuday.

Aidha Kidabuday aliongezea kuwa ameondoka kwa nia njema na amewashukuru wajumbe wote na kuahidi kuwaunga mkono katika utendaji wao wa kazi.

Kamati tendaji ya shirikisho hilo imemteua Ombeni Zavara kukaimu nafasi hiyo hadi hapo uongozi utakapo mtangaza katibu mkuu atakayekuja kuchukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi.

Ikumbukwe mwaka 2012, Gidabuday alijipatia umaarufu mara baada ya kuahidi kuchoma vyeti vyake moto kama timu ya taifa ya riadha ingefanikiwa kurudi na medali katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika jijini London, England.

Baada ya miaka miwili, Kidabuday alifanikiwa kuchaguliwa kuwa mtendaji mkuu wa riadha nchini, mara baada ya kumshinda Gidamis Shahanga kwenye uchaguzi wa chama hicho na kuunda safu ya uongozi akiwa na Anthony Mtaka ambaye alikuwa Raisi wa shirikisho hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

error: Content is protected !!