Saturday , 10 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Baraza la Habari: Wanahabari waachwe huru
Habari MchanganyikoTangulizi

Baraza la Habari: Wanahabari waachwe huru

Spread the love

BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limeitaka serikali kuhakikisha wanahabari wanatekeleza majukumu yao kwa uhuru. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wito huo umetolewa na Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji wa MCT, leo tarehe 2 Novemba 2019,  ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kukomesha uonevu dhidi ya Wanahabari.

Taarifa ya baraza hilo inaeleza kuwa, wanahabari wakichwa huru na kutimiza majukumu yao bila hofu, wataisaidia serikali kutekeleza azma yake ya kupambana na ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma.

“Pia watambue kuwa, bila kuwapo uandishi wa aina hiyo hakuna atakayebaki salama, maana waovu hawatakuwa na cha kuhofia na maliasili za taifa hazitabaki salama, kwani wahusika hawatakuwa na hofu ya kufichuliwa kwa wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka,” linaeleza tamko la MCT na kuongeza;

“Tunaamini wanahabari na vyombo vya habari vikiachwa vifanye kazi katika mazingira huru, bila kuwapo vitendo vya uonevu wataweza kuchangia vizuri katika azma ya serikali ya kupambana na ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma.”

MCT imeeleza kuwa, wakati Tanzania inaadhimisha siku hiyo, wanahabari takribani 72 kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wamekumbwa na mikasa wakati wakitimiza majukumu yao, katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Oktoba 2018 hadi mwisho wa mwezi Oktoba 2019.

Baraza hilo limelaani ukiukwaji huo, na kueleza kwamba matukio ya wanahabari kupigwa, kunyang’anywa vifaa vyao vya kazi, kunyimwa taarifa, kukamatwa, kutishwa na kufungiwa kwa vyombo vyao, yamekuwa ni matukio ya kawaida, pasina wahusika kuchukuliwa hatua.

“Yapo matukio mengine mengi ya unyanyasaji dhidi ya wanahabari, na uingiliaji wa utendaji wa vyombo vya habari hapa nchini ambayo hayakuripotiwa rasmi na waathirika. Pia, yapo ambayo yaliripotiwa lakini hayakuwahi kuchunguzwa na vyombo vya dola na wala wahusika kuchukuliwa hatua,” imeeleza taarifa hiyo ya MCT.

Aidha, MCT imewataka wanahabari kuendelea kuripoti matukio yote ya ukiukwaji wa haki za wanahabari, pamoja na kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

BiasharaTangulizi

TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari

Spread the love  CHAMA cha wanasheria Tanzania (TLS), kimejitosa katika sakata la...

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

error: Content is protected !!