Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kamera 14 za NIDA zilizoibwa zakamatwa
Habari Mchanganyiko

Kamera 14 za NIDA zilizoibwa zakamatwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto
Spread the love

JESHI la Polisi, Mkoa wa Dodoma leo 22 Julai 2019 limefanikiwa kukamata kamera 12 ambazo ni mali ya Mamlaka ya Vitamburisho vya Taifa (NIDA). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kamera hizo, ziliibiwa na ofisa usajili wa NIDA na kuziuza kwa vijana ambao ni wapiga picha.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema, jeshi hilo limekamata vifaa hivyo pamoja na mtuhumiwa.

Muroto alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Ezekiel Subugo (24), ambaye ni msajili wa NIDA anayetuhumiwa kutumia vibaya nafasi yake.

“Mbinu aliyotumia ni kutumia nafasi yake kuiba ofisini na kuuzia watu mitaani, uhalifu huu ni mbaya hasa unapohusisha mtumishi wa umma. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani,” amesema Kamanda Muroto.

Katika hatua nyingine, Mussa Pungu maarufu kwa jina la Mussa Nyela amekamatwa na kete 132 za dawa za kulevya aina ya heroini.

Amesema, mtuhumiwa Nyela kwa muda mrefu ameharibu vijana wengi kwa dawa za kulevya katika mtaa wa Hazina, jijini Dodoma. Mtuhumiwa na wenzake wanne watafikishwa mahakamani.

Pia jeshi hilo limemkamata Rajabu Kambi (32), mkazi wa Area “A” kwa kufanya udanganyifu, akijifanya askari polisi na kutishia watu kwa silaha bandia.

Kamanda Muroto amesema, mtuhumiwa alikutwa na sare ya polisi ‘janglegreen’, bastola bandia na picha akiwa kwenye na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!