Sunday , 5 May 2024
Home Kitengo Michezo JWTZ kushiriki mashindano ya majeshi duniani
Michezo

JWTZ kushiriki mashindano ya majeshi duniani

Kanali Joseph Bakari, Mwakilishi wa Baraza la Michezo la Majeshi Duniani (CISM)
Spread the love

JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), linatarajia kushiriki michezo ya majeshi ya dunia itakayofanyika nchini China kuanzia tarehe 18 hadi 27 Oktoba mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Kanali Joseph Bakari, Mwakilishi wa Baraza la Michezo la Majeshi Duniani (CISM), wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 3 Julai 2019, jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia kuhusu maandalizi ya michuano hiyo Kanali Bakari amesema, JWTZ imeandaa mikakati thabiti itakayowezesha timu zake zitakazoshiriki zinashinda.

Kanali Bakari amesema, JWTZ itashiriki michezo 3 kati ya 27 ikiwemo mchezo wa masumbwi, mieleka na riadha.

“Tanzania tulikuwa tunafanya vizuri katika michezo miwili, boxing na riadha kwa wakati huo. Tunatarajia kushiriki katika michezo mitatu ambayo ni ngumi, mieleka na riadha.

“Mìkakati inafanyika, ukiangalia takwimu ni kweli tulikuwa hatufanyi vizuri, tunalichukua na kuweka mkakati na sisi tufanye vizuri,” amesema Kanali Bakari.

Amesema, dhumuni la michuano hiyo ni kutumia michezo kama njia ya kueneza amani duniani badala ya vita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!