Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Prof. Mbarawa aokoa Sh. 250 mil za sherehe Mwanza
Habari Mchanganyiko

Prof. Mbarawa aokoa Sh. 250 mil za sherehe Mwanza

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Makame Mbarawa (aliyesimama)
Spread the love

WaAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Professa Makame Mbarawa ameagiza Sh. 250 milioni zilizokuwa zimetengwa na wizara hiyo kwa ajili ya sherehe za uzinduzi Wakala wa maji Safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) kupelekwa katika miradi ya maji vijijini. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo leo wakati wa makabidhiano ya usimamizi wa mradi wa maji kutoka halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwenda kwa Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Mwanza (Mwauwassa). 

Amesema amedai kusikitishwa kuona kiasi kikubwa cha fedha kutengwa kwa ajili ya kufanya sherehe za RUWASA wakati kuna maeneo mengine yakikabiliwa na ukosefu wa maji.

Prof. Mbarawa amesema wakala huo umeundwa kwa ajili ya kutatua matatizo ya maji kwa wananchi na wala siyo kuleta matatizo kwa wananchi.

“Leo asubuhi nimeambiwa kuna hela wametenga kiasi cha Sh. 250 milioni kwa ajili ya sherehe zao, sasa nasema ujinga huu hautafanyika mbele ya Mbarawa.

“Watu wanakaa wanatenga hela kwenda kulala hoteli na kukaa wanakula, na lengo letu ni kuona hela zetu tunazopata zinaenda kwa wananchi kufanya kazi na sio kufanya sherehe,” amesema Prof. Mbarawa.

Katika hatua nyingine, Mbarawa amemuagiza katika mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo, kuhakikisha kijiji cha Shilima chenye watu 7,526 na Kaya 1,158, mradi wake wa maji unakamilika ndani ya siku 60.

Waziri Mbarawa amefikia hatua hiyo baada ya mradi wa maji unaogharimu kiasi cha Sh. 2  bilioni kuchukua miaka mitano kutokukamilika hatua ambayo imesababisha wananchi wa kijiji hicho kukosa maji safi na salama.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (Mwauwassa), Mhandisi Anthony Sanga, amesema muda uliotolewa na Waziri huyo watahakikisha wanakamilisha kwa wakati.

Mhandisi Sanga amesema mradi huo umeshindwa kukamilika kutokana na uzembe wa mkandarasi kushindwa kutekeleza majukumu yake na kuilazimu halmashauri ya Kwimba kuvunja mkataba Februari 2018.

“Baada ya mkataba kuvunjwa majadiliano yalifanyika na ushauri kutoka wizara ya maji ambapo mkandarasi alirudishwa kazini Oktoba 2018 na kupewa muda wa miezi sita hadi Machi 30, mwaka huu, ambapo pia alishindwa tena na mkataba ukavunjwa,” amesema Mhandisi Sanga.

Awali akisoma risala mbele ya Waziri Professa Mbarawa Mhandisi wa Maji wa Ruwasa wilaya Kwimba, Boaz Pius amesema vijiji vya Shilima, Mhande na Izizimba “A” ni kati ya vijiji 119 vinavyounda wilaya ya Kwimba na ni kati ya vijiji 12 vilivyopo katika utekelezaji wa programu ya maji na usafi wa Mazingira vijijini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

error: Content is protected !!