JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), linatarajia kushiriki michezo ya majeshi ya dunia itakayofanyika nchini China kuanzia tarehe 18 hadi 27 Oktoba mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).
Kauli hiyo imetolewa na Kanali Joseph Bakari, Mwakilishi wa Baraza la Michezo la Majeshi Duniani (CISM), wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 3 Julai 2019, jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia kuhusu maandalizi ya michuano hiyo Kanali Bakari amesema, JWTZ imeandaa mikakati thabiti itakayowezesha timu zake zitakazoshiriki zinashinda.
Kanali Bakari amesema, JWTZ itashiriki michezo 3 kati ya 27 ikiwemo mchezo wa masumbwi, mieleka na riadha.
“Tanzania tulikuwa tunafanya vizuri katika michezo miwili, boxing na riadha kwa wakati huo. Tunatarajia kushiriki katika michezo mitatu ambayo ni ngumi, mieleka na riadha.
“Mìkakati inafanyika, ukiangalia takwimu ni kweli tulikuwa hatufanyi vizuri, tunalichukua na kuweka mkakati na sisi tufanye vizuri,” amesema Kanali Bakari.
Amesema, dhumuni la michuano hiyo ni kutumia michezo kama njia ya kueneza amani duniani badala ya vita.
Leave a comment