Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge alalamika wabunge kukatwa posho
Habari za Siasa

Mbunge alalamika wabunge kukatwa posho

Spread the love

KHATIBU Said Haji, Mbunge wa Konde (CUF) amelalamikia kitendo cha wabunge kukatwa fedha zao za vikao vya bunge kiholele. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Akiomba mwongozo bungeni tarehe 20 Juni 2019, baada ya maswali na majibu Haji amesema kuwa, anasimama kwa mujibu wa kanuni ya 68 (7) kuomba mwongozo kwamba, kwanini wabunge wamekuwa wakikatwa fedha zao za vikao vya bunge bila kuwashirikisha wabunge?

“Mheshimiwa Naibu Spika Jana tumelipwa fedha za vikao vya bunge lakini cha kushangaza zimekatwa bila sisi kujua na bila utaratibu, na kila mmoja akileta matatizo yake au ya wapiga kura wake ni makubwa mmo sasa ni kwa utaratibu gani tunakatwa fedha zetu ovyo bila kuwa na utaratibu,

“Mheshimiwa Naibu Spika kutokana na hali hiyo naomba mwongozo wako ili Mheshimiwa Naibu Spika tueleze nikwanini tunakatwa fedha zetu bila utaratibu na bila ridhaa yetu ukizingatia kila mbunge ana matatizo yake na wapiga kura wake na tukisema kila mmoja alete wapigakura wake kuja kuleta shida zake ni wengi ”amehoji Haji.

Akijibu mwongozo huo Naibu Spika Dk. Tulia Akson amesema kuwa hakuna mbunge ambaye anaweza kukatwa fedha zao kiholele bali kinachofanyika ni wabunge kukubaliana na hoja ambazo zinatolewa na wabunge pale ambapo wanakuja wageni.

“kumekuwa na tatizo la wabunge kuunga mkono pale inapotokea wageni na kutokea mbunge akatoa hoja ya kutaka mgeni huyo achangiwe,kutokana na hali hiyo ifike wakati sasa inapotekea mgeni akaja bungeni na akatokea mbunge akatoa hoja ya kutaka ngeni huyo hachangiwe wabunge mnaweza kuikubali hoja hiyo au kuikataa,

“Lakini waheshimiwa wabunge nilazima tuelewane kuwa hakuna ofisi ambayo inaweza kukata fedha ya mbunge bila ridhaa yetu au kiholela hivyo sasa nilazima wabunge tuwe makini katika kukubaliana na hoja kwa kuikubali au kuikataa” amesema Dk.Tulia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!