Friday , 2 June 2023
Habari za SiasaTangulizi

NEC yasalimu amri

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesalimu amri baada ya malalamiko ya mara kwa mara kutoka vyama vya upinzani na wanaharakati nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Imeeleza kuwa, wakurugenzi wa hamashauri hawatasimamia chaguzi zozote kama ambavyo vifungu cha 7 (1) na 7 (3) vinavyowapa mamlaka kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Kauli hiyo imeelezwa na Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa NEC akizungumza na wanahabari na kwamba, hukumu ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam iliyopiga marufuku wakurugenzi hao.

Vyama vya upinzani na wanaharakati mbalimbali, wamekuwa wakipinga matumizi ya vifungu hivyo wakieleza kuwa, vinakiuka Katiba ya nchi.

Vifungu hivyo vinawataja wakurugenzi wa majiji, manispaa na wilaya kuwa wasimaizi wa uchaguzi kwa kutumia vifungu hivyo. Hata hivyo Jaji Kaijage alisema, mahakama ilitekeleza wajibu wake hivyo NEC haioni sababu ya kutumia kanuni hizo.

Awali, baada ya mahakama kutoa hukumu ya kupiga marufuku wakurugenzi kusimamia chaguzi, Dk. Adelardus Kilangi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) alisema, wakurugenzi watasimaia uchaguzi huku wakiendelea kukatia rufaa hiyo.

Kauli hiyo ilipingwa vikali na wanasiasa pia wanaharakati mbalimba kwamba, iwapo wakurugenzi watasimamia uchaguzi kama alivyosema AG, watakuwa wamedharau Katiba hivyo kuibua mgogoro.

Prof. Abdalla Safari, Mwanasheria Mahiri wa Mahakama Kuu alisema kuwa, Iwapo NEC itasimama na kauli ya AG, basi itakuwa imejiingiza katika mgogoro kwa kuwa, itakuwa imedharau mahakama waziwazi jambo ambalo halikubaliki.

Jaji Utungamile Ngwala wa Mahakama Kuu alibatilisha vifungu hivyo tarehe 10 Mei 2019, katika kesi namba 8 ya mwaka 2018. Kesi hiyo ilifunguliwa na Bob Chacha Wangwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Jaji Ngwala alisema kuwa, vifungu hivyo ni batili na ni kinyume na Katiba ya nchi. Kwenye kesi hiyo Bob Wangwe aliwakilishwa na Wakili Fatma Karume ambapo ushahidi wa majina 74 ya wakurugenzi kuwa ni makada wa CCM ulitolewa.

Hata hivyo, hivi karibuni Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, alieleza kuwa Kamati Kuu ya chama hicho imewaagiza wanasheria wake kufungua kesi ya kuomba tafsiri ya hukumu ya Mahakama Kuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

error: Content is protected !!