SERIKALI imesema vipimo vya homa ya Dengue vitatolewa bure kwa wananchi katika vituo vya afya na hospitali za umma. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Hayo amesema Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo tarehe 21 Juni 2019 Bungeni Jijini Dodoma wakati akizungumzia hali ya mlipuko wa ugonjwa huo.
Aidha, Ummy amesema serikali itaendelea kuboresha matibabu kwa wagonjwa wa Homa ya Dengue, kwa kuhakikisha dawa za kutosha zinapatikana kwenye vituo vya afya sambamba na kuwajengea uwezo wataalam wa afya.
Hadi sasa, takribani vifo vinne vimeripotiwa kutoka kwa wagonjwa 4,320 waliogundulika kuwa na ugonjwa hu katika mikoa kadhaa, huku Jiji la Dar es Salaam likiwa na wagonjwa 4,029.
Leave a comment