Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwili wa Dk. Mengi kuwasili Jumatatu, kuzikwa Alhamisi
Habari MchanganyikoTangulizi

Mwili wa Dk. Mengi kuwasili Jumatatu, kuzikwa Alhamisi

Michael Ngalo, Mwanasheria wa Familia ya Dk. Reginald Mengi, akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu Kinondoni, Dar es Salaam
Spread the love

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi, unatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu wiki ijayo, kutoka Dubai,  Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mwanasheria wa Familia ya Marehemu Dk. Mengi, Michael Ngalo ametoa kauli hiyo nyumbani kwa marehemu leo tarehe 3 Mei 2019 wakati akitoa ratiba ya shughuli za mazishi ya Dk. Mengi ambaye alikuwa mfanyabiashara mkubwa nchini.

Wakili Ngalo amesema, Dk. Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 2 Mei 2019, ataagwa siku ya Jumanne tarehe 7 Mei 2019 kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Na kwamba, baada ya mwili wa Dk. Mengi kuagwa, siku ya Jumatano tarehe 8 Mei 2019 utasafirishwa kuelekea Machame wilayani Moshi, Kilimanjaro.

Akitangaza ratiba hiyo nyumbani kwake Kinondoni leo, Wakili Ngalo amesema, ibada ya mazishi itafanyika siku ya Alhamisi katika Kanisa la KKKT, Kisereni na kisha kuzikwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

error: Content is protected !!