Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wananchi wafunga ofisi za serikali ya mitaa
Habari za Siasa

Wananchi wafunga ofisi za serikali ya mitaa

Spread the love
WANANCHI wa Kata ya Rutende wilayani Uyui mkoa wa Tabora wamefunga ofisi za serikali ya kata hiyo wakipinga uongozi uliopo kwa madai kwamba hauwasaidii. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).
Tukio hilo limetokea leo tarehe 12 Aprili 2019 ambapo wananchi hao waliifunga ofisi wakishinikiza uongozi uliopo uondolewe na wachaguliwe viongozi wengine.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Gifti Msuya alilazimika kwenda kuzungumza na wananchi hao katika ofisi za Serikali ya Rutende zilizoko katika Kijiji cha Itaga ili kusuluhisha mgogoro huo.
Wakati akizungumza na wananchi hao, Msuya aliwataka watendaji wa kata hiyo kuwajibika kwa wananchi ili kuepuka migogoro isiyo na lazima.
Aidha, Msuya amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia hatua mkononi badala yake wafuate vyombo husika vya maamuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!