Spread the love

MKUU wa Jeshi la Sudan, Awad Ibn Auf aliyeongoza mapambano ya kumng’oa madarakani Rais wa nchi hiyo, Omar al-Bashiri amejiuzulu katika wadhifa wa uongozi wa Baraza la Jeshi linalo ongoza nchi hiyo katika serikali ya mpito ya miaka miwili. Inaripoti Mitandao ya Kijamii…(endelea).

Ibn Auf ambaye ni Waziri wa Ulinzi SudaN, ametangaza uamuzi huo leo tarehe 13 Aprili 2019 kupitia luninga ya taifa hilo, na kumtangaza msaidizi wake Luteni Generali, Abdel Fattah Abdelrahman Burhan kuwa kiongozi mpya wa Baraza la Jeshi linaloongoza taifa hilo.

Vyombo vya habari vinaeleza kuwa, waandamaji walimpinga Ibn Auf kuwa kiongozi wa baraza la uongozi la jeshi ,wakimtuhumu kwamba alikuwa ni mtu wa karibu na Rais aliyeng’olewa madarakani, al-Bashir.

Nchi ya Sudan kwa sasa iko katika miezi miatu ya dharula huku ikiongozwa na Jeshi katika serikali ya mpito ya miaka miwili.

Kwa mujibu wa jeshi hilo, katika kipindi cha usimamizi wake utafanyika mchakato wa marekebisho ya katiba ya nchi hiyo,  huku likiahidi ufanyikaji wa uchaguzi wa huru na wa haki ili kupata serikali ya wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *