Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais wa madaktari; Mishahara haitukidhi
Habari Mchanganyiko

Rais wa madaktari; Mishahara haitukidhi

Spread the love

RAISI wa Madktari nchini Dk.Elisha Osati, ameiomba serikali kuongeza mishahara kwa watumishi wanaotoa huduma kwenye sekta ya afya nchini ili kumudu mahitaji ya maisha. Anaripoti Faki Sosi, (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE Dk. Elisha Osati amesema kuwa, kwa sasa serikali inatoa mishahara kwa wakati.

“Kwa sasa tunapata mishahara kwa muda muafaka labda kwa waajiriwa wapya ambao pia wanapata mishahara yao kwa muda tu ingawa kunachangamoto ndogondogo,” amesema.

Na kwamba, licha ya mishahara kulipwa kwa wakati  ameeleza kuwa,  bado kiwango cha mishahara hiyo haiendani na namna wanavyoitumikia kada hiyo.

“Kwa kweli mishahara haitoshi hivyo nafikiri ukiongea na daktari yoyete au mafanyakazi yoyete wa sekta ya afya, atakwambia  mishahara haitoshi kwa namna tunavyofanya kazi na muda tunaotumia kutoa huduma za afya,” amesema Dk Osati na kuongeza;

“Bado tunaiomba Serikali  na tunaamini bado inanafasi ya kuongeza mishahara lakini sio serikali tu hata mashirika binafsi hospital, binafsi ambayo kuna madaktari bado tunaomba lipokewe hilo sisi kama  chama cha madakrari tunaangalia weledi wa kitaaluma wa madaktari na huwezi kuzungumzi weledi bila kuzungumzia ustawi wa madaktari”.

Amesema kuwa, amemshukuru Rais John Magofuli na Serikali yake kwa kujali kada hiyo ikiwa pamoja kwa kushughulikia matatizo ya madakri kwa muda muafaka.

Tazama video kamili hapo chini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!