February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mgeja amfuata Lowassa CCM

Hamisi Mgeja, akizungumza na waandishi wa habari juu ya maamuzi yake ya kurudi CCM

Spread the love

HAMISI Mgeja, swahiba wa Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu, leo tarehe 6 Machi 2019 ametangaza kurejea  katika Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mgeja ambaye aliondoka CCM Agosti 2015 muda mchache baada ya Lowassa, jina lake kushindwa kupitishwa na Kamati Kuu ya CCM kuwa mgombea urais mwaka 2015.

Wakati akihama CCM Mgeja alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Shinyanga.

CCM sio baba yangu si mama yangu, Watanzania wanahitaji mabadiliko wasipo yapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Ndiyo maneno aliyoyatumia Mgeja alipokua kizungumuza na waandishi wa habari jijini Dar wakati akihama CCM.

Leo akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mgeja amesema, Rais John Magufuli anatekeleza demokrasia.

Amesema, anarejea CCM kwa kuwa, Rais Magufuli anasimamia misingi ya demokrasia kwa kuchanganya wapinzani kwenye serikali yake.

“Sababu kubwa ya kurudi CCM ni jinsi Magufuli (Rais Magufuli) anavyoisimammia demokrasia vizuri kama kuwateuwa wakina Anna Mgwira, Patrobas Katambi, David Kafulila, Kitila Mkumbo.

“Wote hawa walikuwa wapinzani, sasa mnataka demokrasia gani?” Amehoji Mgeja.

Mbele ya waandishi wa habari Mgeja amehoji, kama Rais Magufuli anapigania nchi ikae vizuri kwanini usimuunge mkono

“Kama Afrika na wazungu wanampongeza, sasa kwanini usimuunge mkono?” Amehoji.

Mgeja amechukua hatua hiyo ikiwa ni siku chache baada ya swahiba wake Lowassa kurejea CCM.

Lowassa alirejea CCM tarehe 1 March 2019 akipokewa na Dk. Magufuli, Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Kwenye mapokezi hayo, Lowassa alizungumza maneno machache kwamba “nimerudi nyumbani.”

Hata hivyo, ameahidi kuzungumza na vyombo vya habari siku yoyote kuhusu kilichomkimbiza Chadema.

error: Content is protected !!