Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Michezo Serengeti Boys kujiuliza kwa Australia
Michezo

Serengeti Boys kujiuliza kwa Australia

Kikosi cha Serengeti Boys wakiwa katika mazoezi mepesi wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Australia
Spread the love

BAADA ya kupoteza kwa bao 1-0 mbele ya Guinea kwenye mchezo wa kwanza wa kundi A, timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys itajiuliza tena mbele ya Australia kwenye mchezo wao wa pili utakaochezwa juni 6, 2019 kwenye michuano ya ya UEFA assist. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Goli pekee la Guinea kwenye mchezo huo lilifungwa na Conte Osky kwenye kipindi cha kwanza ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo nakufanikiwa kuondoka na alama tatu.

Baada ya mchezo huo kukamilika kocha mkuu wa Serengeti Boys, Oscra Mirambo alisema kuwa timu haikuwa vizuri kipindi cha kwanza lakini tulikuwa bora sana kipindi cha pili baada ya kufanya marekebisho na alitumia mchezo huo kama kipimo.

“Tuna amini huu mchezo ulikuwa ni kipimo kizuri licha ya mazingira kutubana, kama uwanja kujaa maji lakini mwisho wa siku kuna vitu vingi chanya ambavyo tumevichukua kutoka kwenye mechi hii lakini bado kuna changamoto nazotakiwa kutatua,” alisema kocha huyo.

Mchezo unaofuata wa Serengeti Boys itakuwa Machi 6 dhidi ya Australia na kumaliza mechi ya mwisho kwenye kundi hilo dhidi ya mwenyeji Uturuki Machi 8.

Timu hiyo ambayo ipo nchini Uturuki kwenye michuano hiyo ambayo imeandaliwa na kusimamiwa na Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) inatakiwa kushinda michezo hiyo miwili iliyobaki ili iweze kufuzu kwenye hatua ya robo fainali.

Timu hiyo imekwenda kushiriki michuano hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa COSAFA 2018 nchini Botswana na kupata mwaliko wa kwenda kushiriki michuano ya UEFA assist inayoaandaliwa na shirikisho la mpira wa miguu barani ulaya (UEFA).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!