Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yawasilisha hoja 10, Mahakama kutoa maamuzi J’tatu
Habari za Siasa

Serikali yawasilisha hoja 10, Mahakama kutoa maamuzi J’tatu

Spread the love

SERIKALI imewasiliasha hoja 10 kesi ya kupinga Muswa wa Sheria ya vyama vya siasa iliyofunguliwa na Zitto Kabwe Kiongozi wa ACT-Wazalendo wa Wenzake. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Waombaji wengine ni Joran Bashange Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wanachi (CUF) Bara na Salim  Biman Mkuregenzi wa Mawasiliano ya Umma (CUF).

Moja ya hoja zilizowasilishwa na serikali kuwa Katiba ya Nchi imegawa mamlaka na kuyaheshimu.

Akiongoza jopo la Mawakili , Wakili Mkuu wa Serikali Mark Mulwambo mbele ya Jaji Benhajo Masoud ameeleza kuwa muhimuli wa Mahakama hauwezi kuingilia Muhimili wa Bunge katika kujadilia mambo yake.

Wakili ameleza kuwa amahakama inaweza kujadili sheria iliyotungwa na Bunge sio muswada ambao haujapitishwa kuwe sheria.

Hoja nyengine ya Serikali ni kwamba waombaji wamewasilisha maombi yao kwa kiapi chenye udhaifu ambao hakuna mahala kinapoeeleza muombaji namba moja Zitto .

Kiapo hiko hakina siani ya Zitto ambapo kina upungufu ambapo kimeambatanisha saini ya waombaji wawuli tu ambapo wametaka kwa udhaifu huo kesi hiyo iondelewe Mahakamani hapo.

“Muswada sio sheria mpaka usainewe ndio uweze kuwa sheria kwa sasa Bunge liachwe lifanye kazi yake kisheria na kwamba huo muswa haupo kwenye Ofisi ya Waziri mkuu wala Ofisi ya Mwanasheria Huu Muswada upo bungeni,” ameleeza.

Ameeleza kuwa wabunge wanauwezo wa kutoa maoni ya marekebisho bungeni kwa kuwawakilisha wananchi.

Upande wa watoa maomba uliongozwa na Wakili Mpare Mpoki umekitaka kifungu cha ibara ya 5 kwenye katiba inayoipa mahakama mamlaka ya kutengeu sheria au hatua yoyote itakayochukuliwa na Serikali au Mamlaka yoyote kwa kikiuka haki, uhuru na wajibu kama ilivyoanisha ibara ya 12 hadi 29  kwenye katiba.

Uamuzi  wa Kesi hiyo utatolewa Jumatatu tarehe 14 Januari mwaka 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!