Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli agoma kuzungumza na wapinzani
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli agoma kuzungumza na wapinzani

Spread the love

RAIS wa Jamhuri, Dk. John Pombe Magufuli, “amegoma” kuzungumza na vingozi wenzake wa vyama vya siasa, akidai kwamba “waweza kumteketeza.” Anaripori Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza wakati wa hafla ya upokeaji wa ndege ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL), Rais Magufuli alisema, “siwezi kukutana na kuzungumza na watu wanaonitukana”

Alikuwa akijibu kauli iliyokuwa imetolewa na kiongozi wa Kanisa Kuu la Full Bible Gospel Fellowship Church, Askofu Dk. Zakary Kakobe.

Askofu Kakobe alimtaka kiongozi huyo, kukutana na viongozi wenzake wa vyama vya siasa ili kujadiliana na kubadilishana mawazo kwa mustakabali wa taifa.

Rais alisema, “nimesikia kauli ya Baba Askofu Kakobe. Sina tatizo, lakini unawezaje kukutana na watu wanaokuombea mabaya. Watu wanaokutukana. Watu wanakuombea uchinjwe; unaweza kuhisi kuwa ukikutana nao, hayo yanayosemwa yatatekelezwa.”

Katika hafla hiyo, iliyofanyika kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JKN), jijini Dar es Salaam, Dk. Magufuli alipokea ndege ya tano ya kampuni hiyo.

Ndege hiyo iliyopokelewa na rais, ni aina ya Air Bus 220-300.

Katika hatua nyingine, rais Magufuli ameagiza mamlaka usafiri wa Anga kuzibadilisha matumizi na kuzipaka rangi ya ATCL ndege tatu zinazotumiwa na rais.

“…ndege hizi za rais ambazo ziko tatu, zitapakwa rangi ya Air Tanzania ili ziwe zinabeba abiria. Siku ambazo hazifanyi kazi za serikali, badala ya kuzipaki, zifanye kazi huko. Hiyo ndio Tanzania ninayoitaka,” amesema.

Aidha, Rais Magufuli ameagiza ndege ndogo ya ATCL ambayo imeharibika kwa sasa, ikarabatiwe ili kuongeza idadi ya ndege za shirika hilo.

Rais Magufuli ameeleza kuwa serikali imenunua ndege nyingine takribani mbili ambazo zinatarajiwa kuwasili nchini mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka 2020 na kwamba ndege hizo zikiwasili, ATCL itakuwa na jumla ya ina ndege tisa.

Akizungumzia utendaji ndani ya kampuni hiyo, Rais Magufuli ameagiza watendaji wa ATCL kuwa na mikakati ya kujiendesha kwa faida, ikiwemo kwa kupunguza matumizi ya ovyo.

Amesema, “ninatoa wito kwa ATCL mpunguze matumizi ya ovyo, kila biashara mnayofanya iwe ya faida na si ya hasara. Miaka ya nyuma ATCL tuliyokuwa nayo kuliwa na wafanyakazi, ndege inatumwa Dubai kufuata nguo za maduka ya watu. Tunataka kuwa na shirika linalojiendesha kwa faida.”

Kuhusu ununuzi wa ndege hizo, Rais Magufuli amesema ununuzi huo utaifanya ATCL kutoa ajira kwa watu takribani 380; na inatarajia kuajiri marubani 60 ambapo mpaka sasa tayari wako 50.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!