Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli akabidhi ndege zake kwa ATCL
Habari za Siasa

Rais Magufuli akabidhi ndege zake kwa ATCL

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameagiza ndege mbili kati ya tatu zilizo chini yake, kukabidhiwa kwa Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ili zianze kubeba abiria. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 11 Januari 2019 jijini Dar es Salaam, wakati akihutubia katika mapokezi ya ndege ya tano ya ATCL aina ya Air Bus 200-300, akisema kwamba, kuliko ndege hizo kukaa bila kutumika kutokana na yeye kutosafiri sana nje ya nchi, ni bora ndege hizo zisafirishe Watanzania na watalii.

Kufuatia kauli hiyo, Rais Magufuli ameagiza mamlaka husika ambayo ni Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini kubadilisha matumizi na kuzipaka rangi ya ATCL ndege hizo, ili zianze kufanya kazi.

“….Ndege hizi za rais ambazo ziko tatu, zitapakwa rangi ya Air Tanzania, hizi ziwe zinabeba abiria, siku ambazo hazibebi huku kwetu zibebe WatAzania. Rais huku kwetu kwanza hatembei tembei ,hizo ndege zitapakwa rangi ya Air Tanzania ili zibebe Watanzania. Ili kusudi katika ndege za Tanzania ziwe za kutosha zibebe Watanzania na watalii waingie, hiyo ndio Tanzania ninayoitaka,” amesema Rais Magufuli.

Vile vile, Rais Magufuli ameagiza ndege ndogo ya ATCL ambayo haifanyi kazi kutokana na kuharibika, ikarabatiwe ili kuongeza idadi ya ndege, ambapo ikikarabatiwa shirika hilo litakuwa na idadi ya ndege saba.

Rais Magufuli ameeleza kuwa, serikali imenunua ndege nyingine takribani mbili ambazo zinatarajiwa kuwasili nchini mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka 2020, na kwamba ndege hizo zikiwasili, ATCL itakuwa na jumla ya ina ndege tisa.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameagiza watendaji wa ATCL kuwa na mikakati ya kujiendesha kwa faida, ikiwemo kwa kupunguza matumizi ya ovyo.

“Wito kwa ATCL kwanza mpunguze matumizi ya ovyo, kila biashara mnayofanya iwe ya faida na si ya hasara, miaka ya nyuma ATCL tuliyokuwa nayo kuliwa na wafanyakazi, ndege inatumwa Dubai kufuata nguo za maduka ya watu. Tunataka kuwa na shirika linalojiendesha kwa faida

Kuhusu ununuzi wa ndege hizo, Rais Magufuli amesema ununuzi huo umepelekea ATCL kutoa ajira kwa watu takribani 380, na kwamba ununuzi huo umesaidia Watanzania wengi.Amesema ATCL inatarajia kuajiri marubani 60 ambapo kwa sasa wako 50.

“Mafanikio ya ndege hizi sita, ni ushuhuda tosha wa nguvu za Watanzania, ndugu zangu Watanzania hongereni sana, ndege hizi ni zenu, nawahakikishia Air Tanzania ni shirika linalomilikiwa kwa asilimia 100 na waanchi wa Tanzania, na ndio maana ndugu zangu nawapongeza sana, na hii ndio faida ya kulipa kodi, jukumu la sisi viongozi ni kuhakikisha kodi inatumika ipasavyo isipotee,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!