March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi Yanga waota ‘mbawa’

Makao Makuu ya Klabu ya Yanga

Spread the love

KAMATI ya Uchaguzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), umesoga mbele uchaguzi wa klabu ya Yanga uliokuwa ufanyike siku ya kesho 13 Januari, 2019 katika ukumbi wa bwalo la Maofisa wa Polisi uliopo Masaki, Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya shirikisho hilo haikueleza bayana sababu za kusogeza mbele uchaguzi huo lakiini taarifa kamati hiyo itatoa taarifa kamili siku ya Jumatatu 14 Januari, 2019.

Uchaguzi huo unahailishwa wakati zoezi la kampeni likiendelea huku wagombea mbalimbali wakiendelea kutoa sera zao kwa wanachama wa klabu hiyo ili wapewe ridhaa ya kuongoza timu hiyo.

Wagombea ambao mpaka sasa wapo kwenye kinyang’anyiro hicho katika nafasi ya Mwenyekiti ni Dk. Jonas Tiboroha, Mbaraka Igangula na Erick Ninga. Kwa wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa klabu, waliopitishwa ni pamoja na, Yono Kevela, Titus Osoro na Salum Chota.

Yanga ilipaswa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi baada ya viongozi wao sita wa juu kujiudhuru siku za hivi karibuni akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji, Makamu Mwenyekiti Clement Sanga na wajumbe wanne wa kamati ya utendaji akiwemo Salum Mkemi Hashimu Abdallah, Ayub Nyenzi na Omary Said.

error: Content is protected !!