Monday , 6 May 2024
Home Kitengo Michezo TFF yateuwa waamuzi 82 kuchezesha Ligi Kuu
Michezo

TFF yateuwa waamuzi 82 kuchezesha Ligi Kuu

John Komba, mwamuzi wa Tanzania mwenye beji ya Fifa
Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wamepitisha majina ya waamuzi 82, watakao chezesha michezo mbali mbali ya ligi kuu Tanzania bara katika msimu wa 2018/2019 inayotarajiwa kuanza kesho, huku waamuzi wa kati watakuwa 30, waamuzi wasaidizi 46, na waamuzi 6 waakiba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Uteuzi huo umekuja baada ya kukamilika kwa mtihani wa kupima utimamu wa mwili kwa waamuzi hao uliofanyika mwezi huu Jijini Dar es Salaam ukisimamiwa na chama cha waamuzi nchini pamoja na baadhi ya watu kutoka ndani ya shirikisho la mpira wa miguu nchini.

Majina ya waamuzi waliopitishwa ni Athuman Selukala (Arusha), Erick Onoka (Arusha), Alex Magayi (Dar es Salaam), Elly Sasii (Dar es Salaam), Isihaka Mwalile (Dar es Salaam), Israel Nkongo (Dar es Salaam), Mbaraka Rashid (Dar es Salaam), Nadim Aloyce Leonard (Dar es Salaam) na Liston Hiyari (Dar es Salaam).

Wengine ni Florentina Zabron (Dodoma), Ally Simba (Geita), Amada Simba (Kagera),Jonesia Rukyaa (Kagera), Hussein Athumani (Katavi), Shomari Lawi (Kigoma), Alfred Vitares (Kilimanjaro), Jacob Adongo (Mara), Benedict Magai (Mbeya), Athumani Lazi, (Morogoro), Fikiri Yussuf (Morogoro), Martin Saanya (Morogoro), Abubakar Mturo (Mtwara), Daniel Warioba (Mwanza), Emmanuel Mwandembwa (Mwanza), Ludovick Charles (Mwanza), Ahmad Seif Mbaraka (Pwani), Nassoro Mwinchui (Pwani), Jimmy Fanuel (Shinyanga), Meshack Suda (Singida) na Hance Mabena wa Tanga.

1 Comment

  • Watu wengi tunahitaji koz za urefa,naomba usaidiz naanzeje,maana hatuoni matangazo,Hata kwenye blog za TFF hatuoni tukiuliza hatujibiw why so?vitu muhim ni vp,yaan ada,umri,elimi nk.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

error: Content is protected !!