SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wamepitisha majina ya waamuzi 82, watakao chezesha michezo mbali mbali ya ligi kuu Tanzania bara katika msimu wa 2018/2019 inayotarajiwa kuanza kesho, huku waamuzi wa kati watakuwa 30, waamuzi wasaidizi 46, na waamuzi 6 waakiba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).
Uteuzi huo umekuja baada ya kukamilika kwa mtihani wa kupima utimamu wa mwili kwa waamuzi hao uliofanyika mwezi huu Jijini Dar es Salaam ukisimamiwa na chama cha waamuzi nchini pamoja na baadhi ya watu kutoka ndani ya shirikisho la mpira wa miguu nchini.
Majina ya waamuzi waliopitishwa ni Athuman Selukala (Arusha), Erick Onoka (Arusha), Alex Magayi (Dar es Salaam), Elly Sasii (Dar es Salaam), Isihaka Mwalile (Dar es Salaam), Israel Nkongo (Dar es Salaam), Mbaraka Rashid (Dar es Salaam), Nadim Aloyce Leonard (Dar es Salaam) na Liston Hiyari (Dar es Salaam).
Wengine ni Florentina Zabron (Dodoma), Ally Simba (Geita), Amada Simba (Kagera),Jonesia Rukyaa (Kagera), Hussein Athumani (Katavi), Shomari Lawi (Kigoma), Alfred Vitares (Kilimanjaro), Jacob Adongo (Mara), Benedict Magai (Mbeya), Athumani Lazi, (Morogoro), Fikiri Yussuf (Morogoro), Martin Saanya (Morogoro), Abubakar Mturo (Mtwara), Daniel Warioba (Mwanza), Emmanuel Mwandembwa (Mwanza), Ludovick Charles (Mwanza), Ahmad Seif Mbaraka (Pwani), Nassoro Mwinchui (Pwani), Jimmy Fanuel (Shinyanga), Meshack Suda (Singida) na Hance Mabena wa Tanga.
Leave a comment