Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Upandikizaji figo wazidi kufanikiwa Muhimbili
Afya

Upandikizaji figo wazidi kufanikiwa Muhimbili

Spread the love

IDADI ya wagonjwa waliofanyiwa huduma ya kupandikizaa figo katika hospitali ya Taifa Muhimbili imefikia 19 tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo mwaka 2017. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Hedwiga Swai amesema kuwa utoaji wa huduma hiyo ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa matibabu ambayo yalikuwa hayatilewi ndani ya nchi.

“Tayari wataalam wetu wa ndani hususan madaktari bingwa wamepata ujuzi wa kufanya upandikizaji wa figo kwa kiwango cha asilimia 75 huku asilimia 25 wakielekezwa na wataalam kutoka nje,” amesema.

Aidha Dkt. Swai amesema kuwa wanaahidi kufanya upandikizaji kwa angalau watu watano kwa mwezi ikiwa ni mpango wa muda mfupi kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu ambapo mpango wao wa kila siku ni kufanya upandikizaji kwa mgonjwa mmoja kila siku ambayo ni sawa na wagonjwa 20 kwa mwezi ambapo watakuwa wagonjwa 200 au 240 kwa mwaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!