Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Michezo Dilunga, Feisal Toto waitwa Taifa Stars
Michezo

Dilunga, Feisal Toto waitwa Taifa Stars

Feisal Salum
Spread the love

KOCHA mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Emmanuel Amunike ameita kikosi cha wachezaji 24 kitakachoingia kambini hivi karibuni, kujiwinda na mchezo wa kufuzu Kombe la mataifa afrika Afcon dhidi ya Uganda katika uwanja wa Nelson Mandela ulipo Nambole tarehe 8 Septemba, mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mchezo huo ambao utakuwa wa kwanza kwa kocha huyo mpya kutoka Nigeria baada ya kuchukua mikoba kutoka kwa Salum Mayanga ambaye alikiongoza kikosi hicho kwa kipindi cha mwaka mmoja akitokea Mtibwa Sugar na kuja kumridhi Charles Mkwasa.

Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho pamoja na makipa Aishi Manula, Beno Kakolanya na Mohamed Abdilahaman, kwa upande wa mabeki Shomari Kapombe, Hassan Kesy, Gardiel Michael, Abdi Banda, Kelvin Yondani, Aggrey Morris na Andrew Vicent.

Kwa upande wa viungo kuna Himid Mao, Mudathir Yahya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Simon Msuva, Shiza Ramadhani, Hassan Dilunga, Feisal Salum na Farid Mussa.

Huku kwenye safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Rashid Mandawa, Shabani Chilunda, John Bocco pamoja na mshambuliaji mpya wa klabu ya Tenerife Rashid Chilunda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

Michezo

Kimwanga CUP yazidi kutimua vumbi

Spread the loveMASHINDANO ya mpira wa miguu ya Kimwanga CUP ya kuwania...

error: Content is protected !!