SERIKALI ina mpango wa kuanzisha soko huria la madini (Tanzania Mineral Exchange) ifikapo mwezi Desemba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki wakati akihutubia kwenye kikao cha menejimenti ya wizara ya madini na taasisi zake ambapo wataalamu kutoka Kampuni ya Tanzania Mecantile Exchange PLC-TMC waliwasilisha mada juu ya elimu ya soko la bidhaa Tanzania.
“Natamani kuona ndani ya kipindi cha miezi sita vinavyoweza kufanyika vinaanza kufanyika. Lakini tutazingatia sheria, taratibu na utaalamu kuhakikisha kwamba suala hili linafanikiwa,” amesema Waziri Kairuki.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko alimpongeza Waziri Kairuki kwa kuanzisha wazo hilo ambalo litawezesha kuleta mageuzi katika sekta ya madini, na kuwataka wataalamu wa Wizara ya Madini kulichukulia kwa uzito suala hilo ili utekelezaji wake ufanyike kama ilivyopangwa.
Leave a comment