March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

FIFA yatangaza orodha watakaowania tuzo ya mchezaji bora

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limeweka hadharani orodha ya wachezaji 10 watakaowania tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia kwa mwaka 2018, ambao wanatarajia kupigiwa kura na jopo la makocha pamoja na manahodha wa timu za Taifa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Wachezaji walioteuliwa ni pamoja na Kevin De Bruyne, Eden Hazard, Cristiano Ronaldo, Mohammed Salah, Lionel Messi, Antoine Griezmann, Kylian Mbappe, Harry Kane, Luka Modric na Raphael Varane.

Orodha hiyo ambayo imeongozwa na wachezaji kutoka katika ligi tatu bora ulimwenguni ambazo ni Ufaransa, Uingereza na Hispania ambayo imetoa wachezaji watano, ikifuatiwa na Ligi Kuu Uingereza iliyotoa wachezaji wanne.

Katika hatua nyingine Shirikisho hilo limetoa pia orodha ya makocha 11, watakaowania tuzo ya kocha bora wa FIFA kwa mwaka 2018, huku jina la Gareth Southgate kocha alioiongoza timu ya taifa ya Uingereza kwa mara ya kwanza katika fainali za kombe la Dunia zilizofanyika Urusi likitokea katika orodha hiyo.

Majina mengine yaliotajwa ni pamoja na Massimiliano Allegri, Stabislav Cherchesov, Zlatko Dalic, Didier Deschamps, Pep Guardiola, Zinedin Zidane, Jugern Klopp, Diego Simeone, Roberto Martinez na Ernesto Valverde.

Katika idadi hiyo makocha wanaopewa nafasi kubwa kushinda tuzo hiyo ni Zinedin Zidane aliyekuwa kocha wa klabu ya Real Madrid na Didier Deschamps aliyefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa.

error: Content is protected !!