March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Admin wa WhatsApp afungwa miezi mitano jela

Spread the love

MWANAFUNZI mmoja anayefahamika kwa jina la Junaid Khan (21) ametumikia kifungo cha miezi mitano gerezani nchini India kwa kuwa msimamizi wa kundi la WhatsApp ambalo ulitumwa ujumbe wa matusi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Junaid Khan alishtakiwa kwa kosa la uasi kufuatia kundi hilo kutumwa ujumbe wa matusi huku yeye akiwa miongoni mwa viongozi wa kundi ‘Admin’, hata hivyo alikana kuutuma ujumbe huo.

Adhabu hiyo imemkumba Khan kufuatia sheria ya mitandao nchini India kuruhusu vyombo vya dola kuwachukulia hatua wasimamizi wa makundi ya mitandao ya kijamii au admins ikiwemo kuwafunga gerezani, kwa kosa la kwa kusambaza ujumbe unaoonekana kuwa ni tusi kidini au kisiasa.

Hata hivyo, Polisi inamshikilia admin aliyetoroka kundini kwa madai ya kuhusika kutuma ujumbe huo.

Chanzo: BBC Swahili

error: Content is protected !!