Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ukerewe wachekelea kufikiwa na PSPF
Habari Mchanganyiko

Ukerewe wachekelea kufikiwa na PSPF

Kisiwa cha Ukerewe, Mwanza
Spread the love

WATUMISHI wa umma pamoja na wananchi katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza wameiomba serikali na mashirika yanayotoa huduma za jamii kusogeza huduma zake karibuili kupunguza gharama na muda kwenda mkoani, anaandika Moses Mseti

Wito huo umetolewa katika wiki ya maadhimisho ya huduma kwa wateja ya mfuko wa PSPF ambao umefungua ofisi zake wilayani Ukerewe.

Asilimia 80 ya wananchi wake wanategemea uvuvi kama njia kuu ya kuwaingizia kipato na kuongeza pato na wamekuwa wakifuata huduma ya PSPF jijini Mwanza.

Mmoja wa wananchi hao, ambaye ni mwalimu wilayani humo, Alestida Methew, amesema mara nyingi wamekuwa wakipata wakati mgumu kufuatilia fao la uzazi pindi wanapojifungua kwa kuvuka na meli kutoka visiwani kwenda jijini Mwanza.

“Tumekuwa tukipata usumbufu sana kufuatilia fao la uzazi na unakuta mtu umejifungua mtoto (kichanga) na bado haujapata nguvu za kutembea, lakini kwa sababu ya shida inakulazimu kufika Mwanza kufuatilia lakini kwa ufunguzi huu utatuondolea kero hizi,” amesema Methew.

Mkurugenzi mkuu PSPF, Gabriel Silayo amesema mfuko huo umesogeza huduma zake kwa wakazi wa kisiwa hicho ili kuwaondolea adha watumishi zilizokuwa zikiwakabili ikiwemo huduma za pensheni.

Amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakipokea maoni kutoka kwa wanachama na wadau mbalimbali wakiwaomba PSPF kusogeza huduma zao karibu, hivyo kwa ufunguzi wa ofisi hizo ni utekelezaji wa maombi ya wanachama wao.

“Katika kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na PSPF tunatambulisha mpango wa uchangiaji wa hiari kwa wakazi wa Ukerewe, mpango huu ni fursa kwa Watanzania wote kujiunga na ni kwa watu wote waliopo sekta rasmi na wale ambao siyo rasmi,” amesema Silayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!