February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Albino wakimbilia kwa Rais Magufuli

Walemavu wa ngozi (Albino)

Spread the love

CHAMA cha wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania (TAS) kimemuomba Rais Dk. John Magufuli kutoa tamko la kukemea vikali vitendo vya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ili waweze kuishi kwa amani kama Watanzania wengine,” anaandika Christina Haule.

Mwenyekiti wa TAS , Nemes Temba amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari akikemea kitendo cha ukatili alichofanyiwa mwenzao, Nassoro Msingili (75) mkazi wa kijiji cha Nyarutanga kata ya Kisaki wilaya ya Morogoro vijijini Oktoba 3 mwaka huu.

Temba amesema kitendo cha Msingili kukatwa mkono kimewaumiza sana na anakemea vikali kwa kuwa tayari ameongeza ulemavu mwingine wa kukosa mkono wa kushoto.

Ametoa wito kwa viongozi wa dini, siasa na wadau wengine kutoa elimu kwa umma ili waweze kubadili mitazamo na kuacha kuwadhuru kutokana na kishirikina.

Aidha, aliliomba Jeshi la Polisi likiwa kusimamia usalama wa raia na mali zao kuwalinda watu kama linavyofanya kwa raia wengine.

Ameiomba serikali kufanya sensa ili kupata takwimu sahihi za walemavu wa ngozi kwa lengo la kutoa ulinzi imara dhidi yao.

error: Content is protected !!