KATIKA kuelekea uchaguzi wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baadhi ya wanachama waliochukua fomu kugombea nafasi mbalimbali matumbo yamezidi kupata joto, anaandika Dany Tibason.
Makada hao wanaonekana kujawa na hofu kwa kuwa hawana uhakika kama majina yao yanaweza kurudi hasa kwa wale ambao wanaonekana kuwa na misimamo ya kupinga mwenendo wa chama kwa sasa.
Hofu hiyo imezidi kushika kasi baada ya kauli ya Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali mstaafu, Ngemela Lubinga kueleza kuwa kwa sasa chama kinapitia majina yote ya walioomba nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho.
Lubinga akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliziaka kikao cha CCM na viongozi wa Kikoministi cha nchini Vietnam amesema majina ya waombaji kwa nafasi mbalimbali yameanza kupitiwa.
Amesema majina hayo yatapitiwa kabla ya kuyapeleka katika mkutano mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
“Kwa sasa wapo watu ambao wanapitia majina yote ya wagombea ili kufanya mchujo kulingana na sifa kabla hatujayaingia katika mkutano mkuu ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibunu, ndiyo maana leo umeona tumekuja hapa wageni ambao ni wajumbe wa kamati kuu kutoka chama cha Kikomonisti nchini Vietnam.
“Na amekuja hapa na timu mbalimbali ya utalii na hiyo ni kutaka kudumisha urafiki wetu na wenzetu na wao wanataka kujifunza mambo mbalimbali ya kilimo pamoja na mambo ya kimazingira bila kusahau kushirikishana mambo ya kisiasa” amesema Lubinga.
Leave a comment