Sunday , 3 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Hospitali ya Dodoma yatakiwa kuimarisha wodi ya wazazi
Habari Mchanganyiko

Hospitali ya Dodoma yatakiwa kuimarisha wodi ya wazazi

Selemani Jafo, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Spread the love

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Selemani Jaffo ameuangiza uongozi wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kuhakikisha inaweka mfumo wa hewa ya oksijeni katika wodi za wanawake, anaandika Dany Tibason.

Kadhalika, amemwagiza mkandarasi wa kampuni ya PANCON Intercostruction limited kuhakikisha ifikapo oktoba 20 mwaka huu kuwa imekabidhi jengo la wodi ya kinamama lililopo mjini hapa.

Jaffo amesema lengo la kukamilika kwa wodi hiyo ni kuharakisha huduma ya matibabu kwa wananchi hususani akima mama na watoto na huduma hiyo itasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto.

Mbali na hilo amesema kuwa hospitari ya rufaa ya Dodoma ni kati ya hospitali muhimu kutokana na Dodoma kuwa makao makuu hivyo imekuwa ikipokea wagomjwa wengi wakiwemo viongozi mbalimbali wa kiserikali na wa kisiasa.

Ametoa maagizo hayo alipofanya ziara yake ya kawaida ya kikazi katika hospital hiyo mkoani hapa.

“Dhumuni kubwa la kutembelea hospitali hii ni kwa sababu tuna fahamu wazi Serikali imehamia rasimi Dodoma kwahiyo tunakila sababu ya kuimarisha sekta ya afya na mambo mengi,” amesema.

“Kwa hiyo nimekuja kuangalia hali halisi hasa ya kimiundombinu ya utoaji wa afya, lakini kipindi cha nyuma wakati tunazindua jengo la bima ya afya tulikuwa na bajeti yetu ya mwaka wa fedha kwa hiyo nimekuja kujiridhisha fedha hizo zimetumikaje, lakini nimefarijika ujenzi unaendelea vizuri,’’ amesema

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Dk. Charles Kiologwe amesema changamoto kubwa katika hospitali hiyo ni kukwama kiutendaji

Hata hivyo, Dk. Kiologwe amepongeza serikali kwa juhudi inazozifanya za kutatua changamoto mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Habari Mchanganyiko

TARURA kujenga madaraja 189 kwa teknolojia ya mawe

Spread the loveWakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imejipanga kujenga...

AfyaHabari Mchanganyiko

Majaliwa aipongeza GGML mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining...

error: Content is protected !!