IDADI ya watu waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo yaliyoambata na mafuriko katika mji wa milimani wa Regent nje kidogo ya Freetown nchini Sierra Leone imezidi elfu moja mpaka sasa, anaandika Victoria Chance.
Maporomoko hayo yaliambatana na mvua kali na mafuriko yaliyotokea wiki mbili zilizopita nchini Sierra Leone
Maofisa wa serikali ya Sierra Leone wamesema kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maafa hayo ni zaidi ya elfu moja mpaka sasa hususani kwa kutilia maanani mamia ya watu waliotoweka na hawajulikani waliko hadi hii leo.
Hadi sasa zaidi ya watu 1000 wamethibitika kuwa waliaga dunia kutokana na maporomoko ya udongo ya mji wa Regent. Waziri mkuu wa freetown alitoa takwimu izo
Awali shirika la Hilali Nyekundu la Sierra Leone limetangaza kuwa watu wasiopungua elfu tatu wamepoteza makazi yao kutokana na maafa hayo ya maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji wa milimani wa Regent nje kidogo ya Freetown na kwamba watu wengine 500 hawajulikani waliko.
Jeshi la Sierra Leone na timu za uokoaji zinaendelea na kazi ya kutafuta wahanga wa maafa hayo makubwa.
Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone ameomba misaada ya kimataifa kwa ajili ya wahanga wa maafa ya hayo.
Leave a comment