Sunday , 5 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Magari ya chanjo yatumika kukusanya kodi
AfyaHabari Mchanganyiko

Magari ya chanjo yatumika kukusanya kodi

Magari ya kubeba wagonjwa yaliyotolewa na shirika la umoja wa mataifa Unicef kwa ajili ya halmashauri ya Kakonko
Spread the love

SERIKALI imepiga marufuku halmashauri zote nchini kutumia magari ya chanjo kwa ajili ya kukusanya mapato anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Mvomero, Sadiki Murad (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini gari la chanjo katika kituo cha afya cha Wilaya ya Mvomero linatumika kukusanya mapato licha ya kuwa gari hilo ni chakavu.

Naye mbunge wa Viti Maalum, Sevelina Mwijage (CUF) katika swali lake la nyongeza alitaka kujua ni serikali ina mpango gani wa kupeleka magari mapya ya kubebea wagonjwa katika vituo vya Izimbya na Katekana kutokana na magari hayo kuwa chakavu.

“Kwa kuwa jiografia ya Bukoba Vijijini imekaa vibaya na magari yote ya kubebea wagonjwa ni mabovu lakini gari la kubebea wagonjwa ya wilaya imepelekwa kwenye zahanati ya Kashanje badala ya Katekana Izimbya vijijini je, nivigezo vipi,” alihoji Mwijage.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalim, Saum Sakala (CUF) alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kutengeneza magari yaliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa haraka kutokana na uhaba wa magari unaosababishwa na magari kuwa mabovu.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akijibu swali la nyongeza la Sadiki Muradi (CCM) amesema ni marufuku kwa halmashauri yoyote kutumia magari ya chanjo kwa ajili ya kukusanya mapato kwa halmashauri husika.

“Naziagiza halmashauri zote nchini kuacha mara moja kutumia magari ya chanjo kwa ajili ya kukusanyia mapato na kutokana na hali hiyo tutalazimika kuandika maandishi makubwa ubavuni mwa magari hayo ili yaweze kutambulika haraka,” alisisitiza.

Naye Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jaffo alikiri kuwa magari mengi ya chanjo ni chakavu lakini serikali inaendelea na juhudi za kuona ni jinsi gani ya kuweza kupata magari ambayo yatafaa kufanya kazi ya chanjo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!