Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbunge aibana serikali shamba la NBC
Habari Mchanganyiko

Mbunge aibana serikali shamba la NBC

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Rhoda Kunchele (Chadema) ameitaka serikali ieleze ni lini itakuwa tayari kutatua mgogoro wa shamba lililokuwa likimilikiwa na NBC katika kata ya Kakese Mkoa wa Katavi ili kuwapatia fursa wananchi kuweza kutumia shamba hilo, anaandika Dany Tibason.

Kumchele aliibana serikali kuitaka itoe taarifa wakati akiuliza swali la nyongeza jama bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

“Je ni lini serikali italigawa shamba ambalo lilikuwa likimilikiwa na Benki ya NBC kwa wananchi ili wananchi wa maeneo hayo waweze kujipatia kipato badala ya shamba hilo kuendelea kukaa bila kuzalisha kitu chochote,” alihoji Mkumchele.

Naye mbunge wa Monduli, Juliasi Kalanga (Chadema) aliihoji serikali ni lini itaweza kuyagawa mashamba mengi ambayo yamekaa muda mrefu bila kufutiwa umiliki ili yaweze kutumiwa na wananchi.

“Ni lini serikali itakamilisha mchakato wa kuyafutia umiliki mashamba mengi ambayo yapo Monduli ili yaweze kugawiwa kwa wananchi kwa.

“Mashamba mengi yalifutwa yaliyopo Monduli yalifutwa je ni lini serikali itatoa kauli ni lini itayagawa mashamba hayo kwa wananchi ili waweze kuyatumia,” alihoji Kalanga wakati akiuliza swali la nyongeza.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Siha, Godwin Mollel (Chadema) alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwagawia wananchi mashamba yaliyoko chini ya Hazina kama vile mashamba ya Foster, JourneyEnd na Harlington ili wananchi wayatumie kwa kilimo.

Pia alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kutenga ardhi kwa ajili ya ufugaji kwa wananchi wa Siha ambao kwa sasa hawana maeneo ya malisho kwa mifugo yao.

Akijibu maswali hayo ya nyongeza ya wabunge hao Naibu Waziri wa Ardhi, Nymba na Maendeleo ya Makazi, Angella Mabura amesema kuhusu mgogoro wa shamba la Kakese mkoani Katavi unaweza kutatuliwa na uongozi wa sehemu husika.

Amesema siyo lazima kila mgogoro upelekwe kwenye mamlaka ya Wizara badala yake mkuu wa mkoa, mkuu wa Wilaya au mkurugenzi anaweza kutatua mgogoro huo.

“Migogoro yote siyo lazima wizara ihusike bali mamlaka husika kama vile mkuu wa Mkoa, mkuu wa Wilaya na mkurugenzi wanaweza kutatua migogoro hiyo,” alifafanua Mabura.

Mabura akitoa jibu kwa Kalanga, amesema mashamba mengi ya Monduli yapo katika mchakato wa kufuta rasmi umiliki wa ili kuweza kugawiwa kwa wananchi ili waweze kuyatumia kwa matumizi mengine.

Akijibu swali la msingi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashantu Kijaju, amesema mwaka 2007 serikali ilitoa maelekezo ya kusitisha uuzaji wa mashamba yaliyokuwa hayajabinafsishwa yakiwemo mashamba ya Foster, Journy’s End, Harlington na Kanamodo yaliyopo NAFCO West Kilimanjaro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza Nathwani alivyomshambulia jirani yake

Spread the loveSHAHIDI ambaye ni fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) ameileza mahakama...

Habari Mchanganyiko

DCEA, TAKUKURU waunganisha nguvu kupamba na dawa za kulevya, rushwa

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!