Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara NBC yasaini mkataba na Wizara ya Elimu kusaidia elimu ya ufundi
Biashara

NBC yasaini mkataba na Wizara ya Elimu kusaidia elimu ya ufundi

Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesaini mkataba wa makubaliano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknalojia kwa ajili ya kutoa ufadhili wa masomo ya ufundi kwa vijana wa Kitanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika makubaliano hayo, NBC itaanza kutoa udhamini wa masomo kuanzia mwaka huu 2022 na imetenga jumla ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya programu hiyo mpya.

Wanufaika wa programu watakuwa ni vijana wa Kitanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea na ambao wanatoka katika familia zenye vipato duni. Programu itasimamiwa na Wizara Elimu, Sayansi na Teknalojia na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wataitekeleza.

Ufadhili huo wa masomo unaojulikana kama  NBC Wajibika Scholarship, unalenga kuwapatia vijana ujuzi katika fani mbali mbali ikiwa ni jitihada za kuwafanya waweze kujiajiri na kuajiriwa. Mafunzo yatakuwa yakitolewa na Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA).

Akizungumza katika hafla ya makubaliano hayo leo tarehe 21 Julai 2022, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknalojia, Profesa Adolf Mkenda alisema tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linaweza kutatuliwa kwa kuwasaidia vijana kupata ujuzi ambao utawawezesha kujiajiri.

“Watanzania wengi wana umri kati ya miaka 15 na 45 na Serikali peke yake haiwezi kuwapatia ajira wote. Hata hivyo, kama kundi hili linapatiwa ujuzi sahihi wa kiufundi wanaweza kujiajiri wenyewe na kuwaajiri vijana wengine,” alisema.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa NBC Theobald Sabi alisema Benki hiyo inaendelea kuwekeza kwa jamii. “Tunayofuraha kuwa ushirikianio wetu huu na Serikali kupitia wizara ya elimu utawezesha vijana 1,000 kupata mafunzo ya ufundi na hivyo kuweza kujiajiri”

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, NBC inajivunia kupata fursa ya kuwawezesha vijana wa Kitanzania na kuwapa nafasi ya kutimiza ndoto zao. “Tunawajibu wa pamoja wa kuhakisha tunaliingiza kundi hili kubwa kwenye soko la ajira na kwa msingi huo benki ya NBC inafurahia kuanzisha programu ya ufadhili wa masomo maarufu kama Wajibika Scholarship ambayo itatoa mafunzo ya muda mfupi na kuwapatia vijana ujuzi utakaowasidia  kujiajiri,” alisema. 

Sabi alifafanua kuwa wanufaika pia watafaidika na programu mbali mbali za benki hiyo zitazowasaidia kukua ikiwa ni pamoja na, NBC Kuanasi, Klabu za kibiashara za NBC, ushauri wa kifedha, mikopo na kuunganishwa na masoko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!