Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara RC Senyamule: NMB imetutua mzigo sekta ya afya, elimu
Biashara

RC Senyamule: NMB imetutua mzigo sekta ya afya, elimu

Spread the love

MKUU wa mkoa wa Dodoma (RC), Rosemary Senyamule ameitaja benki ya NMB kama mwarobaini uliowafuta machozi wananchi katika mkoa wake kwenye idara za Elimu na Afya ambako ni kipaumbele cha Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea). 

Senyamule alitoa kauli hiyo juzi wakati akipokea vifaa vya ujenzi vikiwemo mabati, mbao, misumari, viti, meza na makabati kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kati Janeth Shango kwaajili ya shule mbalimbali na Hospitali ya wilaya ya Chamwino.

Vifaa hivyo kwa pamoja vilikuwa na thamani ya Sh43 milioni na vilitolewa kwa shule za Msingi Mizengo Pinda, Chinangali na Dabalo, Shule ya Sekondari Makangwa na Hospitali ya Wilaya ya Chamwino huku benki hiyo ikiahidi kuunga mkono zaidi juhudi za wananchi hasa wanaoanzisha miradi kwa nguvu zao.

Mkuu wa Mkoa alisema vifaa vilivyotolewa na Benki ya NMB vimepunguza mzigo ambao walipaswa kuubeba wananchi na Serikali lakini sasa wanakwenda kufanya mambo mengine baada ya watoto wao kupata madarasa ya kusomea na vifaa mbalimbali.

“NMB mmewatua mzigo wananchi hawa, mmekwenda kugusa maeneo ambayo ni kipaumbele chetu, kwa niaba ya Serikali nasema asanteni sana tena msife moyo kuitazama Chamwino na Dodoma kwa ujumla kwani mngeweza kwenda maeneo mengine lakini mlichagua kwetu,” alisema Senyamule.

Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya mkutano wa wananchi katika shule ya msingi Mizengo Pinda ya Chamwino, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango alisema ni mpango wa benki hiyo kurudisha faida wanayopata kwa jamii.

Shango alisema katika mpango huo, wamejikita zaidi kwenye maeneo ya afya na elimu pamoja na kuchochea maendeleo endelevu na tayari wameanza na kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika upandaji wa miti milioni moja kwa mwaka 2023.

Aidha, Meneja huyo alisema Benki ya NMB inatenga asilimia moja ya faida yake ya mwaka kurudisha kwa wananchi ambapo kwa mwaka huu wametenga Sh4.2 bilioni na kuongeza bilioni 2 zingine kwaajili ya maendeleo endelevu na zingine zikielekezwa  kwenye miradi ya elimu katika shule za msingi na Sekondari pamoja na vifaa vya afya katika hospitali na vituo vya afya.

Awali, Mkuu wa wilaya ya Chamwino, Gift Msuya alisema benki hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa kuchangia utatuzi wa changamoto mbalimbali kwenye jamii ya wanachamwino na wamekuwa ni washiriki wakubwa katika maendeleo ya Chamwino kwa ujumla.

Msuya alisema kila wakati wamekuwa wakikimbilia NMB hasa pale wanapoona mambo yamekwama hivyo akawataka wananchi kuamini eneo salama ni benki hiyo na kuwashawishi kuwa waendelee kufungua akaunti kwani faida kidogo inayozalishwa inawarudia wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

Biashara

Cheza sloti ya Zombie Apocalypse na ushinde kirahisi

Spread the love Wengi wetu hupenda filamu za Mazombie huwa zinatishakidogo lakini...

error: Content is protected !!